Dkt. Mpango: Tumefikia Uchumi wa Kati Lakini Umaskini Bado Upo



Baada ya kula kiapo cha kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema, pamoja na #Tanzania kuwa imeingia kwenye nchi ya Kipato cha Kati lakini bado umasikini ni mkubwa.

Dkt. Mpango amesema ameshuhudia hali hiyo wakati akifanya Kampeni katika maeneo tofauti, amesema, “Bado tunahitaji kufanya kazi kwa bidii na kuwatumikia watu wetu. Fursa bado zipo nyingi na inawezekana ndani ya kipindi kifupi Tanzania ikawa nchi yenye Kipato cha Kati lakini ya Kiwango cha Juu.”

Ameahidi kusimamia nidhamu ya Watumishi walio chini yake, kuondoa uzembe, wizi na ubadhirifu wa mali za Umma huku akiomba watu wazembe wampishe mapema, atende kazi ili nchi isonge mbele.

Ametoa kauli hiyo akishukuru kwa kuchaguliwa tena kuiongoza Wizara ya Fedha, licha ya kuwa alishawaaga Watanzania wakati akisoma bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021, akijua ametimiza wajibu wake na huenda atachaguliwa mwingine.


“Ingawa tupo kwenye uchumi wa kati, huko nilikokwenda kwenye Kampeni umasikini bado ni mkubwa, tunahitaji kuwatumikia Watu ninaamini Rais ukiwa kwenye kitu chako inawezekana Tanzania ikawa Nchi yenye hadhi ya kipato cha kati ila kwa kiwango cha juu, bado tunahitaji kufanya kazi kwa bidii kuwatumikia watu wetu fursa zipo nyingi.

“Mhe. Rais Napenda nikuhakikishie kuwa vita ya kiuchimi ni halisi na mimi nakuahidi kulisimamia hili. Na nichukue fursa hii kuwaomba viongozi wote kila mmoja analipa kodi ipasavyo na tulipe kodi Kama ilivyoelekezwa.

“Naishukuru Familia yangu wakiongozwa na Mke wangu wamekuwa msaada wangu mkubwa wa Sala na Mapenzi nyumbani, namshukuru Mke wangu ameendeleea kunipa raha na utulivu nyumbani, naamini ataendeela kufanya hivyo ili niweze kufanya kazi hii ya Watanzania.

“Wakati nasoma hotuba ya bajeti kwa mara ya 5, Juni nwaka huu, nilikuwa nimewaaga Watanzania nilikuwa najua kwamba nimetimiza wajibu wangu, pengine atakuja mwingine lakini bado Mhe. Rais umenipa imani kubwa inayoenda na wajibu,” amesema Mpango.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad