Donald Trump Afungua Kesi Mahakamani Kupinga Matokeo ya Uchaguzi

 


Maafisa wa kampeni wa rais wa Marekani Donald Trump wamefungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais katika jimbo la Michigan.

Wakati huo huo, Jimbo la Georgia limetangaza kurudia kwa hesabu ya kura jinsi maafisa wa Trump walivyoomba huku rais mteule Joe Biden akiwa anaendelea na mipango ya kupanga utawala wake.

Timu ya kampeni ya rais Trump, imekwenda mahakamani kujaribu kuzuia maafisa wa uchaguzi katika jimbo la Michigan kuidhinisha ushindi wa Joe Biden.

Trump alishinda kura katika uchaguzi wa Michigan, mwaka 2016 lakini akapoteza kwa Biden kwa karibu kura 148,000 katika uchaguzi wa Nov 3.

Biden anaongoza katika jimbo la Georgia kwa kura 14,000 ambalo wademocrat hawajawahi kushinda tangu uchaguzi wa mwaka 1992

Waziri wa mambo ya nje wa Georgia Brad Raffensperger ametangaza kwamba kura zote zilizopigwa zitahesabiwa upya kuanzia wiki hii na matokeo rasmi kuidhinishwa kabla ya Novemba 20, ambayo ni siku ya mwisho kwa shughuli zote za uchaguzi kukamilika katika jimbo hilo.

Kura zitarudiwa kuhesabiwa kwa njia ya mkono na wala sio mashine.

Trump amekataa kukubali kwamba ameshindwa na Biden katika uchaguzi wa urais uliofanyika Nov 3 na badala yake ametangaza kupinga mahakamani matokeo hayo katika kaunti zilizo katika majimbo aliyoshindwa.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Michigan Jake Rollow, amesema kwamba kampeni ya Trump inaeneza madai ya uongo ili kufanya watu wakose Imani na uchaguzi mkuu, akisisitiza kwamba uchaguzi katika jimbo la Michigan ulifanyika kwa njia ya haki na matokeo yake yanaonyesha mapenzi ya wapiga kura.

Wanasiasa maarufu katika chama cha Republican wanamuunga mkono Trump wakisema kwamba ana haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad