HAYA mambo yakuachana halafu mnaanza kuongeleana vibaya mtandaoni si ushamba huu? Haya buana mapema wiki hii aliyekuwa mpenzi (EX) wa msanii wa filamu nchini Aunt Ezekiel, Alfo Alfo ameonekana kumkandia bidada kuwa hafai.
Alfo aliulizwa na shabiki mmoja huko mtandaoni kuwa kwanini aliachana na Aunt, ambapo alijibu kuwa sababu zipo nyingi ila moja ni kwamba mrembo huyo alikuwa anapenda sana kuwatawala wanaume lakini kwake haikuwezekana kwa hiyo ndio maana wakaachana.
“ Aunt like to control men, me Alfo no possible,” aliandika Alfo kwa kimombo.