Watafiti kutoka Australia wamesema wamegundua fuvu la binadamu lenye miaka Milioni mbili nchini Afrika Kusini ambalo litatoa ufahamu zaidi kuhusu mabadiliko ya binadamu.
Fuvu hilo ni la mwanaume linaloitwa Paranthropus robustus, ambalo ni spishi ya ‘binamu’ wa Homo erectus, spishi inayodhaniwa kuwa kizazi cha moja kwa moja cha mababu wa binadamu wa sasa.
Spishi hizo mbili ziliishi katika wakati mmoja, laini Paranthropus robustus walitangulia kufa.
Fuvu hili lilikutwa mita chache kutoka sehemu ambayo fuvu la mtoto jamii ya Homo erectus la miaka kama hiyo liligunduliwa mwaka 2015