Gabriel Sendeu Laiser awa bilionea baada ya kupata madini ya thamani kubwa




Mchimbaji mwingine mdogo wa madini nchini Tanzania ameibuka Bilionea baada ya kupata tani tano za madini ya Rubi yenye thamani ya zaidi ya Shs Bilioni 1.7 kupitia mgodi uliopo eneo la Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha. Akizungumza na Watendaji wa Sekta ya Madini Bilionea Sendeu ametoa shukrani za kipekee kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwathamini wachimbaji wadogo na kuwatetea, hatua ambayo imechangia mafanikio yake.

Mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe amewataka wachimbaji wadogo kuona umuhimu wa kuunganisha nguvu ili waweze kupata vitendea kazi vya kuwawezesha kuchimba kisasa zaidi na kunufaika na rasilimali ya madini ambayo sasa imewekewa utaratibu mzuri wa kuhakikisha yanawanufaisha wazawa. Kwa upande wake kamishna wa madini wa mkoa Arusha Aidan Muhando amempongeza Sendeu kwa kuona umuhimu wa kufanya uchimbaji kwa uwazi na kufuata sheria na taratibu zilizowekwa hatua ambayo imemuwezesha kupata mafanikio yeye mwenyewe , serikali na jamii kwa ujumla .

Gabriel Sendeu Laiser ni kijana wa pili kutoka jamii ya wafugaji wa kimasai kuibuka Bilionea kupitia madini katika kipindi cha kifupi ambapo wa kwanza akiwa ni kijana mwingine Saniniu Laser ambaye alipata kilo zaidi ya 11 za madini ya Tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Shs. Bilion nane.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad