Mbunge wa Arusha mjini, Mrisho Gambo ametangaza neema ya kuwapatia baiskeli, matibabu na huduma nyingine kwa watu 565 wenye ulemavu katika jiji la Àrusha.
Akizungumza katika kikao chake cha kwanza na waandishi wa habari kushukuru baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wajJimbo la Arusha, Gambo amesema amejipanga kuwatumikia vyema wananchi wa Arusha bila kujali tofauti zao.
Gambo amesema baada ya kupata taarifa ya idadi ya wenye ulemavu katika jiji la Arusha kuwa ni 565 na kupokea changamoto za kila mmoja, sasa amejipanga kuanza kushirikiana na wadau wengine kulisaidia kundi hilo.
"Kwa kuanza nitatoa baiskeli 100 za walemavu lakini pia nitalipia bima ya afya kwa walemavu 100 mwaka huu na baadaye tutaendelea"amesema.
Amesema pia tayari kuna mazungumzo yameanza na wataalam kutoka taasisi mbali mbali za afya ili kupawatia matibabu .
Gambo pia ameahidi kuandaaa utaratibu kukutana na makundi mbalimbali kusikiliza kero kila Jumatano na Alhamisi.
Umefanyya la kheri Mrisho,
ReplyDeleteNuizia pia iwe ni Sadaqa ya Marehemu Mama.
Zidisha kuwatumikia wananchi Mungu atakongezea.