Gwiji wa Barcelona, Leone Mess ameripotiwa kutaka mambo mawili kutekelezwa kabla hajafikiria kumwaga wino katika klabu ya Manchester City. Sharti kubwa alitoa mchezaji huyo anataka kuhakikishiwa kuendelea kuwepo Etihad Pep Guardiola na Sergio Aguero.
Messi aliwahi kucheza chini ya Guardiola kwa misimu minne Camp Nou ambako wawili hao walishinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili na la La Liga mara tatu.
Messi ambaye ni mshindi mara sita wa Ballon d’Or pia ni rafiki mkubwa wa Aguero ambaye anacheza naye katika timu ya taifa ya Argentina.
Gazeti la El Chiringuito kupitia SportWitness limedai kuwa, uwepo wa wawili hao Manchester kutachangia kwa kiasi kikubwa uamuzi wa Messi kutua Man City.
Ikumbukwe, Uhusiano wa Messi na Barcelona umeyumba miaka ya hivi karibuni, huku hali ikiwa mbaya zaidi miezi michache iliyopita ambapo aliishtua klabu hiyo nia yake ya kutaka kuondoka.