Geneva ni mji wenye utajiri mkubwa. Ni makao makuu ya benki kubwa za sekta ya kibinafsi. Umoja wa Mataifa na majumba ya mnada ya Sotheby na Christie, ambayo mara kwa mara huuza mawe ya thamani kwa bei ghali sana.
Na mwezi huu mji huo umeanza kutekeleza kiwango cha juu zaidi cha malipo ya chini ya mshahara wa kila mwezi duniani kujibu matakwa ya watu katika kura ya maoni ya ya mwisho wa mwezi Septemba.
Kiwango kimpya cha malipo ya faranga 23 za Uswizi – ambacho ni sawa na euro19, dola 25 ama paundi 22 – kitawapatia watu kiwango cha chini zaidi cha mshahara kuwa euro 3,350.
Kwanini kuna haja ya kufanya hivyo?
Mji huo wa Uswizi huenda ukawa na utajiri mkubwa lakini pia ni nyumbani kwa maelfu ya wafanyakazi wa hoteli, wahudumu wa migahawa, watu wanaotoa huduma za usafi na wafanyakazi wa saluni ambao wanajitahidi kumudu ghara ya juu ya maisha.
Wakati Switzerland ilipoweka amri ya kutotoka nje mwezi machi mwaka huu ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona, picha za milolongo mirefu ya watu waliokuwa wakisubiri kupokea msaada wa chakula mjini Geneva ziligongwa vichwa vya habari.
Watu wanasubiri kupata msaada wa chakula wakati wa janga la corona mwezi Juni 6, 2020 mjini Genevaop
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,Watu wanasubiri kupata msaada wa chakula wakati wa janga la corona mwezi Juni
Mpango huo wa chakula ulikuwepo hata kabla ya janga la corona na bado upo hata baada ya sheria yakutotoka nje kuondolewa miezi kadhaa iliyopita.
Charly Hernandez mshirikishi katika shirika la msaada Colis du Coeur ambalo linagawanya maelfu ya bidhaa za chakula kila wiki katika maeneo ya kati kati ya mji anasema wanawake ndio ndio wanapanga foleni wakiwa na watoto wao kupokea chakula.
Faranga 4,000 kwa mwezi sio?
Huenda ikaonekana pesa nyingi, lakini ikiwa huishi mjini Geneva, Charly anaelezea.
“Chumba kimoja kinakodishwa kwa faranga 1,000 kwa mwezi, ikiwa utafanikiwa kununua chakula kwa faranga 500 kwa mwezi basi wewe ni hodari kwa kubana matumizi, bima ya afya ni 550 kwa mwezi kwa kila mtu. Ukiwa na mke na watoto wawili niambie utasalia na nini.”
Gharama ya maisha mjini Geneva iko juu sana wafanya kazi wengi wanajikakamua kuishi katika mazingira magumu
Gharama ya maisha mjini Geneva iko juu sana wafanya kazi wengi wanajikakamua kuishi katika mazingira magumu
Sheria hii mpya ya malipo inachoweka kiwango cha chini cha mshahara itawasaidia watu wengi, kama Ingrid, ambao wamekuwa wakila vyakula vy abei nafuu migahawani.
“Mwisho wa mwezi mifuko yao inasalia bila kitu,” anasemas. “Nigahawa [hiyo ya chakula] imesaidia sana, kwa sababu watapata ahueni japo kwa wiki moja.”
Hata baadhi ya watu wanaojitolea kufanya kazi, kama Laura, anaona gharama ya maisha mjini Geneva iko juu sana. Japo ni muuguzi hawezi kupata nyumba nzuri ya kuishi mjini hupo.
“Ningelikuwa naishi katiak chumba kimoja kidogo. Sasa bado naishi na wazazi wangu. Nina miaka 26,” anasema.
Nani atakayelipa?
Biashara zinazowalipa wafanyakazi chini ya faranga 23 kwa saa watalazimika kuwaongezea malipo. Hatua ya kutekeleza malipo hayo mapya kati kati ya janga la corona ambalo limechangia kushuka kwa faida itakuwa na athari kubwa, anahofia Vincent Subilia wa chama chama cha wafanyabishara wa Geneva.
“Hoteli na migahawa tayari zinakabiliwa na changamoto kadhaa kutokana na janga hili,” alisema. “Hali ambayo huenda ikasambaratisha uwepo wa sekta hizo.”
Mmoja wa wamiliki wa migahawa, Stefano Fanari, wameambia kituo cha televisheni cha Uswizi kwamba haoni ikiwa atamudu kulipa ada inayotakiwa. Kama mpishi mkuu, marupurupu yake ya mwezi ni kati ya faranga 5,000 na 6,000 kwa mwezi.
“Nitawezaje kuendelea wakati natakiwa kuwalipa waosha vyombo kiasi hicho cha fedha?
“Je nipunguze saaa zao za kufanya kazi? Msinielewe vibaya, Sipingi suala la wao kulipwa 4,000 kwa mwezi. Lakini kwa hali ilivyo hatuwezi kumudu malipo hayo. Nimejitolea, Nafanya kazi hapa kwa saa 12 kwa siku. Nifanye nini?”
Sasa nini kitafanyika?
Mshahara wa chini wa Geneva umeidhinishwa kuwa sheria sio kwa sababu ni hatua iliyowekwa na serikali, bali ni kutokana na pendekezo la wananchi mjini Geneva “mpango wa wananchi”.
Walikusanya saini nyingi kutaka suala hilo lipigiwe kura ya maoni ,na kufikia Septemba tarehe 27 wapiga kura waliitikia ndio, kwa kwa asilimia 58% dhidi ya 42%.
Mfumo wa Uswizi wa demokrasia ya moja kwa moja unamaanisha kwamba wapiga kura wanauamuzi wa mwisho, kiwango cha chini cha mshahara sasa ni wa chini ni lazima.
Place du Molard mjini Geneva
Kuna hofu kwa sekta ya mgahawa na mshahara mpya
Mara nyingi, raia wa Uswizi hupiga kura kwa mikini sana linapokuja suala la matumizi ya fedha za umma. Lkaini siku hiyo hiyo pia waliunga mkono likizo ya wiki mbili ya uzazi kwa mzazi wa kiume ambayo italipwa.
Kwa Charly Hernandez hatua hizi ni dalili njema, hususan nyakati hizi ngumu, kwasababu watu katika people in this largely wealthy country are looking out for one another.
“Walipigia kura, na hilo limenifurahisha sana. Tuna demokrasia ya moja kwa moja na hilo ni jambp zurisana, lakini kile watu wasichokijua ni kwamba juhudi nyingi za kiraia hupuuzwa.
“Ni vyema kwamba mambo yameanza kubadilika na baadhi ya vitu vinaidhinishwa a, kwa hivyo naamini mambo yanazidi kuimarika … Japo kwa mwendo wa pole pole, lakini ndio kasi ya Uswizi.”
Mtihani mwingine kwa wapiga kura utakuja baadaye mwezi huu wakati raia wa Uswizi wataamua kuhusu “mpango wa uwajibikaji wa biashara”.
Mpango huo utazihitaji kampuni zilizo na makao yake Switzerland kuwajibikia kisheria na kifedha ukiukwaji wa haki za kibinadamu katika hatua zote za utendaji wa kampuni hizo mahali popote duniani.
Kura ya ndio kwa pendkezo hilo huenda ikagharimu zaidi ya mshahara ya chini wa Geneva.