Hong Kong yazindua laini ya simu kuripoti uhalifu



Polisi Hong Kong hii leo imeanzisha namba ya simu ya mawasiliano ya moja kwa moja itakayowawezesha raia kuripoti matukio yoyote yanayotishia usalama wa taifa. 

Laini hiyo ya simu itawaruhusu wakazi kutuma taarifa za kijasusi kupitia ujumbe wa maandishi, barua pepe, na App ya Kichina ya WeChat. 


Polisi pia imesema wakazi pia wanaweza kuitumia laini hiyo ya simu kutuma picha, video na sauti. Hatua hiyo imekosolewa vikali na makundi ya kutetea haki za binadami, yakidai itaongeza mgawanyiko uliotanda mjini humo. 


Vikundi vya kutetea haki za binadamu vimesema hatua hiyo itakandamiza uhuru wa kujieleza, katika wakati ambapo serikali ya China bara imeanzisha sheria tata ya usalama ya kitaifa huko Hong Kong.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad