1. Unahangaika kwa sababu umeshindwa kuchaguliwa kuingia Chuo Kikuu - Hukupata passmarks za kutosha. wenzako wengi wamechukuliwa hata uliokuwa unawadharau! Umechoka, unayatazama majengo ya chuo kikuu kwenye taarifa ya habari. Unatamani ungekuwa mwanachuo kama wao -
2. Kuna mwingine alichaguliwa kuingia chuo, kamaliza na ufaulu mzuri mno. Huu ni mwaka wake wa nne hajapata kazi anazunguka mtaani na vyeti vizuri kabisa, kaaply kila nafasi za ajira zaidi ya 100 sasa, katika hizo aliitwa mara moja tu kwenye usaili, na hakuchaguliwa. Anamtamani mtu aliye ajiriwa -
3. Aliyeajiriwa amechoka! Ana madeni kila taasisi mshahara wake kila mwezi unaishia kulipa madeni na nauli ya kwendea kazini. Anaishi kwa kudra za Mungu tu. Kila siku saa 11 anaamka kuwahi daladala vinginevyo atafika kazini kwa kuchelewa. Anamtamani Boss ambaye kila siku hupaki V-8 lake jeusi hapo nje ya ofisi yao.
4. Boss amejaa wategemezi kibao, matarajio ya jamii kwake ni makubwa. Anavaa suti tu kulinda jina lake - Lazima awe na gari kubwa zuri, nyumba nzuri, watoto awapeleke shule za gharama apende sipende kwa sababu lazima aishi kulingana na matarajio ya jamii. Akienda kwenye misiba lazima achangie hela ndefu, nyumbani kwao wanamsema kwa sababu hajawajengea wazazi wake nyumba nzuri - Hana hamu, kachoka na mawazo anafukuzia fedha za kukidhi aina ya maisha aliyonayo - Anatamani angeacha kazi akawa mfanya biashara mwenye utajiri.
5. Mfanya biashara tajiri amejaa mambo mengi kichwani - Hajawalipa mishahara watumishi wake mwezi wa tatu sasa, miradi inaelekea kufilisika, hana amani. mwezi uliopita wafanyakazi waliandamana kugoma na akaahidi kujitahidi kulipa - hiyo hela anaitoa wapi? anawaza. TRA wametishia kuzifungia amali zake iwapo hatalipa madeni mwezi ujao. Anawaza wapi apate hela. Machoni pa jamii ni kibosile fulani, ana magari kadhaa kwake, watoto matawi- wanarukaruka tu beach..hawajui kichwani anafikiria kujinyonga. Anatamani angekuwa mtu maskini anayekula mlo mmoja lakini hasumbui kichwa namna hiyo.
6.Mtu masikini naye anatamani naye awe tajiri....nacheka kweli. Na wewe unalaumu nini?