Human Rights Watch yaitaka Saudi Arabia kuwajiibishwa katika mauaji ya Khashoggi



 Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch leo limetoa wito kwa wanachama ishirini wa kundi la nchi 20 zilizoongoza kiuchumi duniani G20 kuishinikiza Saudi Arabia kuwaachia huru wanaharakati waliozuiliwa kinyume cha sheria. 

Human Rights Watch vile vile inataka Saudi Arabia iwajibike kwa dhuluma ilizozifanya katika miaka iliyopita. 


Shirika hilo limeyasema haya kuelekea mkutano wa G20 utakaofanyika kwa njia ya video katika nchi hiyo ya kifalme baadae mwezi huu. 


Kama mwenyekiti wa sasa wa kundi hilo Saudi Arabia imejaribu kulinadhifisha jina lake baada ya malalamiko kutoka kote duniani kufuatia kuuwawa kinyama kwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, kuzuiliwa kwa wanaharakati wa haki ambao ni wanawake na kuhusika katika mzozo wa kivita nchini Yemen. 


Saudi Arabia haijatoa tamko lake bado kuhusiana na wito huo wa Human Rights Watch.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad