ICC: Majeshi katika Operesheni ya Libya yalitega mabomu majumbani

Umoja wa MataifaMwendesha mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu - ICC Bi Fatou Bensouda ameripoti jana kuwa operesheni ya karibuni iliyoshindwa ya vikosi vya mashariki wa Libya ilihusisha mtindo wa machafuko na matumizi ya mabomu ya kutegwa ardhini ya wanajeshi waliokuwa wakirudi nyuma yaliwaumiza raia na huo ni uhalifu wa kivita wakati vinapotumiwa kiholela. 

Bensouda ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa kuna taarifa za kuaminika kuhusu matumizi ya mabomu ya kutegwa ardhini na vifaa vingine vya kulipuka. Amesema watu wasiopungua 49 waliuawa na mabomu ya ardhini kati ya Aprili na Juni mwaka huu. 


Ameongeza kuwa taarifa za karibuni zinaonesha jeshi la mashariki likiongozwa na kamanda Khalifa Hifter vilifanya mashambulizi ya kiholela ya angani na kuyalipua maeneo ya raia, utekaji nyara kiholela, kuwazuilia na kuwatesa watu, mauaji ya kiholela, watu kupotea na uporaji wa maji ya raia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad