Idadi ya Wanaume Wenye Umri wa Kufanya Kazi Waliojiua Yaongezeka

 


Wizara ya Afya ya Japani imesema kuwa wanaume 705 walio na miaka ya 20 hadi 50 walijiua mwezi Septemba mwaka huu. Idadi hiyo imeongezeka kwa watu 56 au asilimia 8.6 ikilinganishwa na mwezi huo mwaka jana.


Idadi ya mwezi Agosti mwaka huu ilikuwa ni 706, au asilimia 6.6 zaidi ya ile ya mwezi Agosti mwaka jana.


Wizara hiyo imesema wanawake 640 walijiua Septemba mwaka huu, na kuzidi idadi ya mwezi sawa na huo mwaka jana kwa mwezi wa nne mfululizo.


Taasisi isiyo ya kujipatia faida ya Lifelink yenye makazi yake jijini Tokyo imesema wanaume wengi hukaa na matatizo yao bila ya kutafuta mashauriano.


Shimizu Yasuyuki anayeongoza taasisi hiyo amesema kuwa janga la virusi vya korona linawaathiri mno wafanyakazi wasio waajiriwa wa kudumu na wale waliojiajiri, na kuwa serikali inapaswa kuchukua hatua za kulinda ajira zao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad