Idadi ya watu waliokufa katika maandamano Uganda wafikia 45




Polisi nchini Uganda imesema kuwa idadi ya vifo vya vilivyotokea katika maandamano ya wiki iliyopita imeongezeka na kufikia watu 45.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu, msemaji wa polisi Fred Enanga, amesema waliokufa ni wanaume 39 na wanawake sita.

Chombo kimoja cha habari nchini humo kimevinukuu vyanzo vya usalama vikisema kuwa ufyatuaji mkubwa wa risasi ulifanywa na watu ambao hawakuwa wamevaa sare, ambao walirekodiwa na umma wakinadi bunduki kwenye mitaa.

Waandamanaji walikuwa wakidai kuachiliwa huru kwa Bobi WineImage caption: Waandamanaji walikuwa wakidai kuachiliwa huru kwa Bobi Wine

Waziri wa usalama nchini humo Jenerali Elly Tumwiine aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa kuwa polisi na vikosi vingine vya usalama wana haki ya kufyatua risasi na kuua. Kama waandamanaji "wanafikia kiwango fulani cha ghasia ."

Polisi ilisema kuwa maafisa wa polisi 11 walishambuliwa na kujeruhiwa na waandamanaji.

Maandamano yaliibuka katika maeneo mbalimbali katika mji mkuu Kampala, huku waandamanaji wakitoa wito wa kuachiliwa huru kwa mgombea wa urais Robert Kyagulanyi, al maarufu Bobi Wine, ambaye alikuwa amekamatwa katika mkutano wa kampeni.

Baada ya kushikiliwa kwa siku mbili mahabusu, alishitakiwa kwa kukiuka sheria za kudhibiti virusi vya corona, na kupewa dhamana. Kwa sasa amerejea katika msururu wa kampeni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad