IGP Sirro: Watu 254 wako mahabusu kwa sababu ya uchaguzi mkuu

 


Dar es Salaam.  Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amesema vijana 254 wanashikiliwa na jeshi hilo wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali wanayodaiwa kuyafanya kipindi cha Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.


IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo Novemba 19, 2020 Jijini Dar es Salaam alipozungumza na wanahabari kuhusu tathmini ya kiusalama kupitia uchaguzi mkuu huo, akidai kuwapo kwa watu waliojaribu kuharibu uchaguzi huo ili nchi isitawalike hususani visiwani Zanzibar, walikofanikiwa kudhibiti vurugu. 


“Nimekuwa nikiwaambia vijana siku zote, kwamba usikubali kuingia kwenye mtego halafu wenzako wakakuacha unapata shida wewe na familia yako, nafikiri hayo niliyosema sasa wanayaona kwa sababu kuna watu 254  wako mahabusu,” amesema Kamanda Sirro.


Amewahoji vijana anaodai kuwa wanashikiliwa kwa makosa hayo kuwa; “Baadhi ya viongozi waliosababisha hayo wako wapi, wamewaachia shida, taabu. Wanasema sikio la kufa halisikii dawa.”


Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera Sirro na wana ulinzi n Usalama.
    Usiwaonee muhali walla Haya, Wote waliokkuwa na lengo la uvunjifu wa Amani na Utulivu wa nchi yetu Bara na Visiwani.

    Tukianzia na Viongozi waoo wa ngazi za Juu za Jitoo na Mtowe
    na BoniJako na Godiless na Ponda Mwalimu mwinika Tungundu alisepa na walitayarishwa kuhakikisha Matairi yanachomwa na
    Vilipuzi vya Mazilui vinalipuliwa kwa Mshindo.

    Mungu ameinusuru nhi yetu na sasa ni kuwashughulikia.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad