Ikulu ya Marekani Yawekewa Uzio Kuhofia Waandamaji Wakati wa Uchaguzi



Mamlaka nchini Marekani imejenga tena uzio kuzunguka Ikulu ya Marekani, siku moja kabla ya uchaguzi wa Rais, huku ukiwa na hofu kuwa kutakuwa na maandamano ya watu wengi, machafuko ya wenyewe kwa wenyewe na hata uasi wa silaha.

Huku kukiwa na dhana kwamba matokeo ya uchaguzi hayatajulikana mara moja na watu wa Chama cha Republican kujitangazia ushindi mapema au kuleta changamoto za kisheria kupinga matokeo ya uchaguzi kama Rais Donald Trump ataonekana kushindwa.


Kizuizi hicho kitaunda mzunguko wa mraba kuzunguka Ikulu, uzio kama huo uliwekwa wakati wa maandamano ya kitaifa dhidi ya ukatili wa Polisi na ubaguzi wa rangi baada ya mauaji ya George Floyd, Mmarekani mwenye asili ya Afrika.


Hali ya Marekani kuwa na wasiwasi wakati wa uchaguzi na mgombea kukataa matokeo haijawahi kufikirika hapo awali.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad