Iwapo Donald Trump Atakataa Kuondoka Ikulu, Nini Kitatokea ?


Katika historia ya miaka 244, hakujawahi kuwa na rais ambaye amekataa kuondoka Ikulu baada ya kushindwa kwenye uchaguzi.

Ubadilishanaji wa madaraka kwa njia ya amani, yenye mpangilio na kisheria ni jambo ambalo linatambulika katika demokrasia ya Marekani.


Kwa sababu hii, Rais Donald Trump alitangaza kuwa amekataa kukubali kuwa ameshindwa kwenye uchaguzi na Joe Biden na kusababisha hali ambayo haijawahi kushuhudiwa kabla.


Na pia hali hiyo imefanya wachambuzi kuanza kufikiria matukio ambayo hayajawahi kufikirika kwamba yanaweza kutokea kabla.


“Bado matokeo ya uchaguzi hayajakamilika”

Trump alikuwa akicheza gofu nje ya mji wa Washington DC Biden alipotangazwa kuwa ameshinda Novemba 7 na vyombo vikuu vya habari nchini Marekani.


Muda mfupi, timu ya kampeni ya rais ilitoa taarifa na kusisitiza kuwa “bado matokeo ya uchaguzi hayajakamilika”.Donald Trump playing golf.


Trump alikuwa akicheza gofu Biden alipotangazwa mshindi

“Sote tunajua kwanini Joe Biden anakimbilia kujionesha kuwa mshindi, na kwanini vyombo vya habari ambavyo ni washirika wake vinajitahidi kwa kila namna kumsaidia: hawataki ukweli ujitokeze,” alisema kwenye taarifa.

“Ukweli ni kwamba matokeo ya uchaguzi huu bado hayajakamilika,” taarifa hiyo iliendelea akionesha kwamba Trump ataendelea kupinga matokeo ya uchaguzi kwa kuwasilisha kesi mahakamani, akidai kuwa kuna wizi wa kura.

Katiba ya Marekani imeweka wazi kabisa kuonesha kuwa muhula wa sasa wa rais anayeongoza unamalizika Januari 20″.

Joe Biden alifanikiwa kushinda majimbo ya kutosha kumuwezesha kupata zaidi ya kura za wajumbe 270 zinazohitajika ili mgombea aweze kuwa rais.

Hivyo basi, ana haki ya kuongoza kama rais kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Donald Trump bado kuna vyanzo na njia za kisheria anazoweza kuzitumia kupinga matokeo ya uchaguzi lakini pengine kuwe na mabadiliko makubwa mahakamani siku zijazo na pia aweze kuthibitisha kuwa kweli uchaguzi umekumbwa na udanganyifu na wizi kama ambavyo amekuwa akidai bila kutoa ushahidi wowote.

Lakini kinachofahamika mpaka sasa ni kwamba Januari 20 ndio tarehe ambayo Rais mteule anachukua rasmi madaraka – na pia ndio siku ambayo Trump ni lazima ajiuzulu.Trump with his team in the White House's Oval Office

Kipi kitatokea ikiwa Trump atakataa kuondoka White House?

Nafasi ya Urais

Trump amekuwa akionya katika kipindi chote cha kampeni kuwa hatakubali kushindwa.


Alisema mara kadhaa kwamba amedhamiria kusalia madarakani, bila kujali watakachosema mamlaka za uchaguzi na kuashiria kuwa anaweza tu kushindwa ikiwa kura zitaibwa.


Kwahiyo nchi imeanza kuzungumzia suala la ikiwa Trump atatimiza tishio lake na kujaribu kukatalia madarakani, je nini kitatokea?

Dhana hiyo pia ilianza kuzungumziwa na Joe Biden wakati wa kampeni yake.

Katika mahojiano ya Juni 11, mchekeshaji Trevor Noah alimuuliza Biden ikiwa amewahi kufikiria kuhusu suala la Trump kukataa kuondoka katika makazi ya rais.

“Ndio, Nimekuwa nikilifikiria,” Biden alijibu, akiongeza kuwa katika hali kama hiyo anadhani jeshi ndio litakalo husika kumzuia kuendelea kusalia madarakani na kumfurusha kutoka Ikulu.

Msisitizo wa Biden kuwa wapiga kura ndio wanaoamua matokeo ya uchaguzi wala sio wagombea kumejirejelea katika kampeni yake Ijumaa: “Watu wa Marekani ndio watakaoamua katika uchaguzi huu, na serikali ya Marekani ina uwezo mzuri kabisa wa kusindikiza wasiohitajika nje ya Ikulu,” taarifa hiyo imesema.

Suala hilo linaweza kutatuliwa na majeshi ya Marekani au Shirika la Kijasusi kutimiza jukumu la kumsindikiza Trump kuondoka kwenye makazi ya rais.

Shirika la Kijasusi lina jukumu la kumlinda rais, lakini pia kisheria lina jukumu la kulinda wote waliokuwa marais na litaendelea kumlinda Trump baada ya Januari 20. 

Akikataa kuondoka huenda huduma ya usalama ikamlazimisha Trump kuondoka Ikulu

Je ni Matukio gani yanayoweza kutokea?

Iwapo Trump atakataa kabisa kutoka madarakani, huenda kukawa na ulazima wa kuangazia uaminifu wa wanajeshi kwa Rais.


BBC imezungumza na wataalamu ikiwa kuna uwezekano wa Trump kujaribu kutumia vikosi vya jeshi kusalia madarakani kinyume na sheria.


“Kwa rais kutumia vibaya madaraka kwa kuamua kusalia madarakani baada ya kupoteza ucgauzi, itakuwa vigumu na pia ni hali ambayo itakuwa inakwenda kinyume na kile ambacho kimekuwa kikizoeleka,” Profesa Dakota Rudesill, mtaalamu wa sera na masuala ya usalama wa taifa mwenye kuhusishwa na chuo kikuu cha Ohio Marekani ameiambia BBC.


“Itakuwa na athari mbaya kwa taifa hilo, kuanzia kanuni za msingi za uhusiano wa raia na jeshi na matarajio ya kidunia katika suala la demokrasia,” alionya.


Hata hivyo, aliweka wazi katika maoni yake kuwa, matukio yanayoweza kutoke ikiwa Trump atang’ang’ania kusalia madarakani kama ataungwa mkono na vikosi vya usalama.


“Wanajeshi walikula kiapo kutekeleza katiba kwa uaminifu na wala sio kuwa muaminifu kwa mwanasiasa aliye madarakani. Na afisa wa juu zaidi jeshini, Jenerali Mark Milley, mwenyekiti wa kamati ya wakuu wa Wafanyakazi wote, amesema mara kadhaa kwamba jeshi halitajihusisha na chochote na uchaguzi huu.”


Profesa Rudesill hayuko peke yake katika kuangazia kinachoweza kutokea, Keisha Blaine ni profesa wa chuo kikuu cha Pittsburgh na mtaalamu wa masuala ya maandamano.


“Ukweli wa kwamba imefika wakati ni lazima tujiulize ikiwa jeshi linaweza kuingilia uchaguzi kunaelezea mengi kuhusu hali ta kusikitisha inayokumba nchi yetu,” ameiambia BBC.


Miaka minne iliyopita, raia wengi wa Marekani hawakuwa na wasiwasi kuhusu hili. Lakini baada ya kumuona Trump akipeleka maafisa polisi na jeshi wa serikali kuu wakati wa maandamano huko Portland na Washington miezi ya hivi karibuni, sasa suala hili limezua wasiwasi. Sioni kama hili linaweza kutokea lakini hatuwezi kuliondoa kabisa katika orodha ya yanayoweza kutokea hasa ukizingatia kilichotokea mwaka huu,” aliongeza.


Katika maandamano yaliyodai kupinga ubaguzi katika ya mwaka, Trump aliamua kupeleka wanajeshi kukabiliana na waandamanaji. 


Maelezo ya picha,Juni mosi, Mark Milley, mwenyekiti wa wakuu wa wafanyakazi, aliandamana na Trump kupiga picha akiwa ameshika Bibilia mita chache kutoka Ikulu huku kukiwa na maandamano ya kupinga kifo cha George Floyd – siku kadhaa baadaye Milley alijutia kuchukua uamuzi huo

Ghasia wakati wa kusubiri kuapishwa kwa rais?

Profesa Rudesill anasema pia naye ana wasiwasi wa kile kinachoweza kutokea.


“Nimeandika kuhusu uwezekano wa Rais Trump kujaribu kutumia amri ya Rais, au Wizara ya Sheria inayodhibitiwa na washirika wake wa kisiasa kujaribu kutoa maagizo yanayoonesha kuwa ngazi ya juu ya uongozi inastahili kuangalia uwezekano wa Trump kuwa mshindi wa uchaguzi wenye utata,” mtaalamu huyo amezungumza na BBC, lakini akaonya kuwa hilo “sio sahihi na halikubaliki.”


“Kuagiza jeshi kuendelea kumtii rais hata baada ya kumalizika kwa muhula wake yaani mchana wa Januari 20 kutaliweka jeshi katika hali tete,” alisema.A Trump follower in Minnesota on 7 November


Wachambuzi wameonya kuwa ikitokea hali mgombea anayeshindwa kwenye uchaguzi anakataa kukubali kuwa ameshindwa “huenda kukatokea ghasia”

“Nusu ya nchi na watu wengine wengi kote duniani watafikiria kuwa jeshi ambalo halistahili kuuunga mkono upande wowote wa kisiasa limechukua msimamo unaoegemea upande mmoja. Jeshi halistahi kabisa kupokea agizo la namna hiyo,” Profesa Rudesill amesema.


Mbali na hali iliyopo ambapo uhuru wa jeshi unawekwa katika mizani kwasababu ya mzozo wa kisiasa, wengine wameonya kuwa hali ya sasa ya kisiasa huenda ikasababisha ghasia katika eneo hilo.


Hali ambayo mgombea urais aliyeshindwa anakataa kukubali matokeo kunaweza kusababisha “uvunjaji mkubwa wa sheria”, Keisha Blaine ameiambia BBC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad