Jamii Yatakiwa Kuondokana na Tabia ya Kujisaidia Vichakani Ili Kujikinga na Magonjwa ya Mlipuko



Na Timothy Itembe Mara.

JAMII imetakiwa kuondokana na tabia ya kujisaidia vichakani kwani kufanya hivyo ni moja ya njia ya kuchochea kuwepo magonjwa ya mlipuko.


Mratibu wa uelimishaji Afya na Afisa Afya wa halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara,Agrey Hyera alisema hayo alipokuwa akihojiana na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya kujikinga na magonjwa ya mlupuko .

Hyera alisema kuwa ili kuondokana na magonjwa ya mlipuko kuna haja  jamii kuondokana na tabia ya kujisaidia vichakani na badala yake wajengetabia ya kujisaidia chooni na choo hicho kiwe Bora.

Afisa huyo aliongeza kuwa hatarajii kuona Bianadamu ambaye anaishi Sayari ya karine ya ishirini na moja bado hana choo cha kujisaidia na badala yake watu wake wanaenda kujisaidia porini jambo ambao ni hatari kwa Afya ikiwemo kueneza maambukizi ya magonjwa ya mlipuko.

“Magonjwa ya mlipuko kama vile kuhara damu magonjwa ya matumbo yote hayo yanatokana na binadamu kula mavi(KINYESI)kwa maana hiyo lazima sasa jamii iondokane na tabia ya kujisaidia porini na badala yake ijenge tabia ya kwenda kujisaida chooni na kufanya hivyo ni moja ya maendeleo”alisema Hyera.

Mtu anapojisaidia vichakani mvua ikinyesha inatiririsha kinyesi kile hadi kwenye mito ambapo watu wanachota maji kwa matumizi ya nyumbani na ukinywa maji yaleyenye kinyesi  lazima upatwe na magonjwa ya kuhara ikiwemo kuumwa matumbo na magonjwa mengine ya Ameeba aliongeza kusema Afisa huyo

Mmoja wa wanawake mjini hapa ambaye hakutaka jina lake kutajwa kwenye vyombo vya habari alisema kuwa jamii haina uelewa wa kutosha juu ya matumizi sahihi ya vyoo jambo ambalo linasababisha watu wengi kwenda kujisaidia vichakani hususani wale ambao wanakaa vijijini.

Mama huyo alioomba serikali kupitia wataalamu wa Afua kuondokana na kutia joto viti vya ofisini na badala yake waende vijijini ili kutoa elimu ya Afya ikiwemo elimu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko.

Mwana mama huyo alisema kuwa jamii ikielimishwa vyema juu ya maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kutasaidia kuokoa rasilimali zinazopotea pindi magonjwa hayo yanapokuwa yamelipuka katika jamii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad