*Baba anapokuwa bado ana nguvu, yuko kazini, ni mkulima, au anafanya biashara*; *huwa anakua na nguvu na ushawishi mkubwa sana kwenye familia yake*: *Familia humsikiliza, humjali humpenda, na huzingatia na kutambua uwepo wake*.!!
*Tatizo huanza pale baba anapozeeka, nguvu za uzalishaji mali zimekwisha, au amestaafu.! Na pale watoto wanapokua wamekua watu wazima wameanza maisha yao*.! *Hapo ndipo mambo kwa baba huanza kuharibika na kupewa kisogo na wanae*.!!
*Mkewe huanza kumchukulia poa! Ile heshima aliyokuwa akipewa huanza kupungua taratiibu*.. *baba hasikilizwi tena Kama zamani, isitoshe anakua hahusishwi sana tena kwenye mambo ya mkewe sababu hata akiambiwa atasaidia nini na pesa hana*? *Badala yake mkewe huanza kuwafanya watoto kuwa washirika wake zaidi na kumuweka kando mumewe*... *Baba anaachwa pembeni*!!
*Mama huanza safari kwenda kwa watoto, huko hukaa sana, baba kaachwa nyumbani peke yake! Watoto wanamgombea mama aende kwao, lakini baba hakuna anayemtaka*!
*Watoto wanasahau kwamba, upendo ulioonekana kwa mama kuanzi , malezi, mavazi, chakula alitafuta baba*.!!
*Elimu yao ilitokana na baba, kupendeza kwao, afya yao ilitokana na baba*.!! *Mama yao kupendeza kwake kulitokana na baba*, *Mama alikuwa mama wa nyumbani, baba alikuwa mtu wa kazini, anatoka alfajiri anarudi usiku amechoka nyang'anyang'a*: *Safari za kibiashara huko na kule *Hakulala nyumbani akiipambania familia*.😭.
*Sasa wakiwa nyumbani na mkewe, simu toka kwa watoto 80% anapigiwa mama*, *Baada ya maongezi mareefu, ndo baba anapewa simu anasalimiwa dk 2 imeisha hiyo*! *Baba simu anayo, ila haoni simu za watoto wakimpigia, na wakimpigia ni kwa sababu maalumu tena maongezi huwa mafupi! Hawana muda nae*!
*Baba anajikuta anakuwa mpweke sana, anakua mgeni kwa familia yake mwenyewe! Wale ambao alizimalizia nguvu zake za ujana kuwatafutia maisha hawana muda nae tena*!😭.
*Wanaanza kuiharibu na kuitenganisha ndoa ya wazazi wao*.😭
*Pale baba anapokuwa anaihitaji sana faraja ya familia yake sababu ameshazeeka*;... *Familia humpa kisogo*! *Upweke unamsonga!*
*Mawazo humsonga, hili hupelekea kinga ya mwili kushuka na kufanya iwe rahisi kushambuliwa na magonjwa na haichukui muda baba anauawa na watoto wake mwenyewe*:😭 *hatimaye, anafariki*!!
*Familia wataliaa, watachapisha matisheti, watatoa mapesa kumnunulia sanduku la gharama na kumjengea kaburi la gharama*. *Mitandaoni watampost sana*! *Lakini alipokuwa hai... No one cares*!
*Hii ni laana kubwa kwa watoto*: *Wanapanda mbegu mbaya ambayo nao watavuna kwa watoto wao*:😭😭
*Wewe mtoto unaye fanya hayo, tubu, acha kabisa*: *Jirekebishe ili ujiponye na laana hii*:
*Tuwajali baba zetu, walijitoa na kujinyima sana kufanya tufike tulipo*! *Ni dhambi mbele za Mungu tena ni laana mbaya kuwapuuza baba zetu*!
*Wakati unaendelea kumsifia mama yako kuwa ni bora, msifie hata baba yako kwakuwa alikuchagulia mama yako aliye bora*.
*Kama umeguswa na darasa hili, share kwa wengine* . *Umebarikiwa*:✋🏾✋🏾.
C&P.