Fuatilia moja ya simulizi ambayo imegonga vichwa vya habari duniani siku za hivi karibuni - jiwe kubwa lilianguka katika nyumba moja kutoka juu ya anga na kumfanya mmiliki kuwa milionea na kubalidilisha maisha yake.
Ilisemekana kuwa jiwe hilo thamani yake ni dola milioni 1.8 na kumfanya mwanaume huyo kuwa milionea ndani ya usiku mmoja tu.
Josua Hutagalung, mtengenezaji wa majeneza katika kijiji cha Sumatra, alikuwa anaendelea na shughuli zake mapema Agosti aliposikia mlio mkubwa wa kipekee kutoka juu- na sekunde kadhaa baadaye - akasikia mlio mkubwa kana kwamba unabomoa nyumba yake.
Mara ya kwanza, Josua aliogopa hata kuangalia ilikuwa kitu gani: kitu hicho kisichojulikana kilikuwa kimeanguka kupitia dpaa ya nyumba yake kwa kasi na nguvu ya ajabu kiasi cha kupasua bati ya upande mmoja na kujikita sentimita 15 chini ya ardhi chini ya sakafu ya nyumba.
Na baada ya mshindo huo akaamua kunyanyua kilichoanguka na kugundua kuwa ni jiwe la uzito wa kilo mbili.
"Nilipoliinua, bado lilikuwa moto moto," alizungumza na mwandishi wa habari wa BBC idhaa ya Indonesian.
"Hapo ndipo nilipoanza kuona ninachokiinua ni jiwe lililoanguka kutoka juu ya anga. Haikuwezekana kuwa mtu alitupa jiwe lile na kulipitisha juu ya la nyumba."
Sio jambo la kawaida kwa jiwe kuanguka kutoka juu ya anga hadi katika paa la nyumba ya mtu na alichofanya Josua ni kuliweka katika mtandao wa Facebook.
Taarifa hizo mara moja zikaanza kusambaa katika kila sehemu ya dunia hadi ngazi ya kimataifa.
Lakini pia kama ilivyotariwa, wanasayansi ndio waliokimbilia jiwe hilo kutaka kujua limetoka wapi, limetengenezwa na nini na lina uvumbuzi gani kuhusu dunia.
Vimondo kama hivyo vinasemekana kuwa na umri zaidi ya miaka bilioni nne.
Hata hivyo kufikia Agosti, hakuna ndege iliyokuwa inaelekea Indonesia kwasababu ya ugonjwa wa virusi va corona.
Hapo ndipo wanasayansi wa Marekani walipowasiliana na Jared Collins, Mmarekani anayeishi Indonesia kuomba awasaidizi katika kufanya mazungumzo na Josua.
Jiwe hilo lilichunguzwa uhalisia wake na pia kama lilihifadhiwa vizuri. Ikiwa lingegusa maji tu lingeharibika haraka.
"Inafurahisha kushika kitu ambacho ni halisi na cha kweli, kitu cha zama za kale, enzi za awali za mfumo wa jua," Mmarekani huyo alizungumza na BBC.
"Lilikuwa na harufu ya kipekee ambayo ni vigumu sana kuelezeka."
Mnunuaji wa Marekani alipokubaliana na Josua bei ya jiwe hilo, hatimaye likauzwa.
Kando na lile jiwa kubwa pia kuliwa na vijiwe vingine vidogo viwili ambavyo viliishia kuuzwa katika mtandao wa Ebay Marekani.
Jiwe kama la Josua linaweza kuwajulisha wanasayansi mwanzo hasa wa maisha duniani.
"Watu hufurahia sana kitu ambacho umri wake ni mkubwa kuliko hata dunia, kitu ambacho kimetoka juu ya anga," Profesa Garvie anaelezea. "kwasababu hiyo kuna watu wanaokuwa tayari kulipa mamia au maelfu ya madola kumiliki kipande kidogo tu."
Mfano wa jiwe lililopatikana na Josua, linawawezesha wanasanyasi kuvumbua uhalisia wa maisha mwanzoni mwa uwepo wa dunia.