Joe Biden Aapa Kuwaunganisha Wamarekani Wote

Joe Biden amesema ni wakati wa kuponya vidonda nchini Marekani katika hotuba yake ya kwanza kama rais mteule , akiapa kwamba hatoligawanya taifa hilo na badala yake ataliunganisha.


Tupatie kila mtu fursa , bwana Biden alisema akiwahutubia wale waliompigia kura.


Bwana Biden alimshinda rais aliyepo madarakani Donald Trump baada ya zoezi la kuhesabu kura lililokumbwa na hisia baada ya uchaguzi wa Jumanne.


Bwana Trump bado hajakubali kushindwa na hajazungumza hadharani tangu kushindwa kwake kulipotangazwa alipokuwa akicheza gofu.


Matokeo hayo yanamfanya rais Trump kuwa rais wa kwanza aliyehudumu kwa muhula mmoja tangu miaka 90.


Kamati yake ya kampeni imewasilisha kiwango kikubwa cha kesi katika majimbo kadhaa lakini maafisa wa uchaguzi wanasema kwamba hakuna Ushahidi kwamba kulikuwa na udanganyifu katika uchaguzi huo dhidi yake.


Sherehe kadhaa zilizuka katika miji mikuu baada ya vyombo vya habari kutangaza kwamba bwana Biden alishinda siku ya Jumamosi.


Wafuasi wa Trump walikuwa wamekasirishwa na matokeo hayo katika baadhi ya miji lakini hakukuwepo na ripoti za matukio yoyote.


Biden: 'Lazima tuwache kuwachukulia wapinzani wetu kama maadui zetu.


Akihutubia wafuasi wake katika eneo la kuegesha magari katika mji wa nyumbani kwake wa Wilmongton ,Delaware, bwana Biden alisema: Naahidi kuwa rais ambaye angependelea kuwaunganisha na sio kuwagawanya, ambaye hatazami majimbo mekundu na ya buluu bali Marekani kwa pamoja.


Bwana Biden ambaye ameshinda kura milioni 74 kufikia sasa , ndiye rais aliyeweza kupata kura nyingi Zaidi za wananchi , aliwapongeza kwa kumuunga mkono lakini pia akazungumza na wafuasi wa Trump moja kwa moja.


Ni wakati kufutilia mbali matamshi makali , kupunguza viwango vya joto na kuonana tena, sikizaneni''. Bwana Bide alisema.


''Na ili kupiga hatua ni sharti tuwache kuwachukulia wapinzani wetu kama maadui''.


Rais huyo mteule, ambaye aliwasili katika jukwaa akivalia barakoa, alitangaza kwamba atabuni kamati yake ya kukabiliana na virusi vya corona ili kuhakikisha iko tayari kuidhinisha maamuzi atakayotoa siku ya kuapishwa kwake mwezi Januari.


Majibu ya utawala wa rais Trump kuhusu mlipuko huo uliokuwa katikati ya kampeni hizo za urais, yalikosolewa pakubwa na Biden . Zaidi ya Wamarekani 237,000 wamefariki , zaidi ya taifa jingine lolote duniani. Bwana Biden atakuwa na umri wa miaka 78 anapochukua madaraka na kumfanya kuwa rais mwenye umri mkubwa zaidi katika historia ya Marekani.


Harris: 'Mulichagua matumaini na umoja '


Bwana Biden alikaribishwa kuwahutubia wafuasi wake na mgombea mwenza , Kamala Harris, ambaye ameweka historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza mweusi na Muhindi Mmarekani kuwa makamu wa urais mteule.


"Wakati ambapo demokrasia yetu ilikuwa hatarini dunia nzima ilikuwa inatazama na mukawapatia Wamarekani siku mpya'', alisema.


"Mulichagua matumaini , heshima sayansi na ukweli - mulimchagua Biden kama rais wa Marekani. Na barabara mbele haitakuwa rahisi lakini Marekani iko tayari na hivyobasi mimi na Joe pia tuko tayari."


''Pia alizungumzia kuhusu matokeo ya urais: Huku nikiwa mwanamke wa kwanza katika ofisi hii sitakuwa wa mwisho''.


 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad