Kama Ulikuwa Hujui Mtu Wangu Hawa ndiyo Wajuba a.k.a Wajumbe Wanao Amua Nani awe Rais wa Marekani

 

               Pichani ni Wajumbe Maalum (2016) wakionesha baadhi ya kura za kumchagua Rais wa Marekani.


Leo tarehe 3 Novemba, taifa la Marekani linapiga kura ya kumchagua Rais wake ambaye ataliongoza taifa hilo kwa miaka minne ijayo

Wagombea katika kinyang'anyiro hicho ni Donald Trump wa chama cha Republican ambaye anawania muhula wake wa pili pamoja naye Joe Bidden wa Democrat ambaye alikuwa Makamu wa Rais katika utawala wa Baraka Obama.


Huu ni uchaguzi wa 57 kufanyika tangu Taifa hilo lipate uhuru wake Julai 1776, uchaguzi huu unatajwa kuwa wa aina yake kutokana na kuvuta hisia, maoni mseto kwa Wamarekani pamoja masalahi ya taifa hilo na washirika wake. Jumla ya watu milioni 211 wamejiandikisha kupiga kura ili kuwachagua wawakilishi wa miji yao, majimbo pamoja na wale wa serikali kuu.

 

Kando na mamilioni ya wapiga kura ambao idadi yao inafika milioni 211 lakini wajumbe wajulikanao kama Electrol College (Wajumbe maalum) hawa ndiyo huamua nani awe Rais wa Taifa la Marekani kutokana na kura zao kuwa za turufu, ambapo jopo lao lina jumla ya wajumbe 538 kwenye majimbo yote, ambapo katika idadi hiyo kuna wawakilishi 435, Maseneta 100 na kuna wawakilishi 3 kutoka Wilaya ya Columbia.


Mgombea urais anahitajika kupata angalau kura 270 za wajumbe maalum ili kuweza kushinda kinyang'anyiro cha urais nchini Marekani licha ya kuwa ameshinda ama kushindwa kura za raia. Kwani historia ya Taifa hilo inaonyesha kuwa wapo Marais kadhaa ambao wamewahi kupata wingi wa kura za wananchi lakini wakaangushwa na kura za wajumbe maalum.


 


Mfano mwaka 2016 mgombea wa Democrat Hillary Clinton alimshinda Trump katika kura za wananchi kwa 2% zaidi, lakini akaangushwa kwa kura za wajumbe maalum ambapo alipata kura 232 huku Trump akipata 306, hivyo kumfanya Trump kuwa Rais wa 48 wa taifa hilo.


Aidha mwaka 2000 Al Gore wa chama cha Democratic dhidi ya George W Bush wa Republican ambapo Bush aliibuka kuwa rais wa Marekani licha ya Al Gore kupata kura laki 5 na elfu 40 zaidi alizopigiwa na wananchi wa Marekani lakini kwa kuwa hakupata idadi kubwa ya kura za wajumbe maalum basi hakuweza kuchukua hatamu za uongozi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad