SHOMARI Kapombe, beki wa kulia mzawa ndani ya kikosi cha Simba ambaye pia jina lake limetajwa kwenye majina ya wachezaji 27 wa Taifa Stars chini ya Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije, amesema kuwa wanaamini watatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu
Simba ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ambao waliutwaa msimu wa 2019/20 baada ya kucheza mechi 38 na kufi kisha pointi 88. Kabla ya juzi Jumamosi kucheza na Yanga, Simba walikuwa nafasi ya tatu wakikusanya pointi 19, huku Yanga wakiwa nazo 23 kwenye nafasi ya pili.
Zote zilikuwa na mechi tisa. Kapombe alisema: “Tuna kazi kubwa ya kufanya kwetu sisi wachezaji kutimiza majukumu yetu ndani ya uwanja, lengo ni kuona tunatwaa ubingwa na ili hilo liwezekane ni lazima tushinde mechi zetu.
“Kikubwa ninawaambia mashabiki waendelee kutupa sapoti katika kazi yetu kwani uwepo wao uwanjani unatuongezea nguvu,” alisema. Kwenye mechi zote tisa ambazo Simba ilikuwa imecheza kabla ya jana, Kapombe alikuwa ni chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu.