Kaze Aanza Kazi ya Pointi Tisa



BAADA ya kumaliza kibarua chake cha kusaka pointi 12 kwenye mechi zake nne za mwanzo, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze ameingia kwenye mtengo mwingine wa kusaka pointi tisa kwenye mechi zake tatu za mwezi Novemba.


 


Ndani ya pointi hizo 12 alifanikiwa kupata pointi nane na kupoteza pointi nne baada ya kupata sare ya bila kufungana dhidi ya Gwambina FC na ile ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Simba.


 


Alishinda mechi mbili ilikuwa bao 1-0 Polisi Tanzania, 2-1 KMC na kumfanya akusanye jumla ya mabao manne na kufungwa mabao mawili ndani ya dakika 360 kwa sasa ana kazi nyingine tatu kwa ajili ya kufunga mwezi Novemba.


 


Mechi hizo itakuwa dhidi ya Namungo iliyo nafasi ya tisa na pointi 14 inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery, Novemba 22, Uwanja wa Uhuru.


 


Kibarua kingine itakuwa dhidi ya vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC yenye pointi 25 baada ya kucheza mechi 10 ikiwa chini ya Aristica Cioaba itakuwa ni Novemba 25.


 


Kaze atafunga shughuli kwa kukutana na JKT Tanzania iliyoanza kuchangamka kwa kuwa inashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi msimu wa 2020/21, ilikuwa dhidi ya Mwadui FC ambapo ilishinda mabao 6-1 chini ya Kocha Mkuu, Abdalah Mohamed,’Bares’ Novemba 28.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad