KADA machachari wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyeangushwa katika nafasi ya ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Ally Keissy amesema haelewi kilichotokea katika uchaguzi huo ambao Aida Khenan wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) alishinda.
Aida ambaye ndiye mbunge pekee wa Chadema aliyeshinda katika uchaguzi huo, alinyakua kiti hicho kwa kura 21,226 huku Keissy akipata kura 19,972.
Aidha, akizungumza na RISASI kwa njia ya simu jana, Keissy alisema hawezi kuzungumzia zaidi anguko hilo kwa sababu wananchi ndio wanaoujua ukweli. “Nenda kafanye upepelezi huko kwa wananchi wa Nkasi utajua kitu gani kilifanyika maana hata mimi sijui kilichotokea.
“Kwa kweli siwezi kusema zaidi kuhusu hayo matokeo nitaonekana muongo, wewe nenda kawaulize watu wa Nkasi utaujua ukweli,” alisema.
Kauli hiyo ya Keissy inaashiria kutokubaliana na matokeo hayo yaliyotangazwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, Missana Kwangura. Matokeo hayo ya Nkasi Kaskazini yaliwashangaza wengi hasa ikizingatiwa kada huyo wa CCM alikuwa mmoja wa wabunge machachari hasa katika kutoa na kuchangia hoja ndani Bunge.
Mbali na Keissy ambaye ameliongoza jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo (2010-2020), kuanguka katika uchaguzi huo, pia Hawa Ghasia ambaye ameliongoza jimbo la Mtwara vijijini kwa muda wa miaka 15 (2005-2020), naye alingushwa huko na Shamsia Mtamba (CUF).
Katika uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu, ni makada hao wawili pekee wa CCM kwa upande wa Tanzania bara walioshindwa katika uchaguzi huo ambao umekiwezesha CCM kunyakua majimbo 256 kati ya 264.
Hata hivyo, vyama vya upinzani Chadema, CUF na ACT Wazalendo viliambulia wabunge nane pekee wa majimbo ilihali katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 vilikuwa na wabunge 116 wa viti maalumu na majimbo.
Keissy Baba.
ReplyDeleteWamekuchakachua, hii ni baada ya makontrakta na wakurugenzi kukuona wewe ni mnoko baada ya kuwachomea.
Cha kufanya kwa sasa:
Washitaki Takukuru , Fungua Jalada kupinga haya.
Magu, ameliona na analijua hilo.
Hao Makontrakta walimaliza kazi..?
Keissy Baba.Wewe ni Mzalendo..!!
ReplyDeleteWamekuchakachua, hii ni baada ya makontrakta na wakurugenzi kukuona wewe ni mnoko baada ya kuwachomea.
Cha kufanya kwa sasa:
Washitaki Takukuru , Fungua Jalada kupinga haya.
Magu, ameliona na analijua hilo.
Hao Makontrakta walimaliza kazi..?