Kesho ni Dar derby watani wa jadi Simba dhidi ya Yanga nini utabiri wako ?



Ni mchezo unaovuta hisia za mashabiki wengi wa soka Tanzania na kwingineko duniani kutokana na ukubwa wa vilabu hivi viwili nchini Tanzania.




Wawili hao wamekuwa wakitambiana kila mmoja akijivunia ubora wa kikosi chake msimu huu mara ya mwisho simba ili iliigaragaza Yanga 4 – 1 kwenye mchezo wa nusu fainali wa kombe la ligi (Azam Federation Cup).


Mara hii Yanga ikiwa chini ya kocha Mrundi Cedric Kaze watakuwa nyumbani kwenye dimba la Mkapa jijini Dar es salaam kuiakaribisha Simba inayonolewa na kocha Mbelgiji Sven Vandenbroeck.

Kaze ameshaiongoza Yanga kwenye michezo minne na kati yake ameshinda mitatu na kutoa suluhu mmoja huku Scven yeye amekuwa na Simba toka msimu uliopita.


Yanga wamezoeleka kucheza mpira ya pasi ndefu na kasi huku Simba wao wakipiga pasi nyingi mpaka golini, kwenye mchezo wa kesho Yanga wanaingia wakivunia kuwa na ukuta imara zaidi wakiwa hawajafungwa mchezo hata mmoja msimu huu huku wakiwa wameruhusu magoli mawili tu.



Simba wao wanaingia kifua mbele wakiwa na safu imara zaidi ya ushambuliaji wakiwa wameshajikisanyia jumla ya magoli 21 mpaka sasa huku watani wao wakiwa na magoli 11 tu.


Mchezo wa kesho utachezeshwa na waamuzi sita wawili wakiwa nyuma ya magoli, mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Almasi Kasongo alitangaza azma hiyo kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya mara kwa mara kutokana na makosa yanayofanya na waamuzi kwenye micheozo ya ligi kuu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad