Wakati ambapo Rais wa Marekani, Donald Trump alifurahia ulinzi wa kipekee wa kikatiba kutokana na hatua za kisheria , iwe ya jinai au ya kiraia unaelekea kukamilika.
Sasa, baada kushindwa uchaguzi wa urais wa mwaka 2020, Bwana Trump hivi karibuni atakuwa raia wa kawaida tena
Hii inamaanisha atapoteza kinga ya rais,hali ambayo itamweka katika
"Atakapotoka ofisini mazingira yatabadilika," Daniel R Alonso, mwendesha mashtaka wa zamani wa Marekani na jimbo la New York ameambia BBC. "Hatakuwa tena na uwezo wala mamlaka ya rais kukomesha uchunguzi."
Bwana Trump anakabiliwa uchunguzi kadhaa wa kihalifu inayokumba kampuni na mashirika yake.
Kando na haya, kuna kesi kadhaa zinazomkabili ikiwa ni pamoja na madai ya udanganyifu uliofanywa mwanafamilia wake hadi unyanyasaji wa kingono uliofanywa na mwandishi wa safu ya ushauri.
Mzozo wa kisheria unatokota. BBC imetathimini jinsi mapambano makuu sita ya kisheria yanavyoweza kutokea.
1) Madai ya malipo ya kuwanyamazisha wapenzi wa zamani
Tunachokijua: Nyota wa filamu za ngono Stormy Daniels, jina halisi Karen McDougal amedai kumekuwa na njama ya kuwanyamazisha wapenzi wa zamani wa Trump
Hii ni kashfa iliyomzonga Trump alipokuwa anajiandaa kungia Ikulu ya White House. Wanawake aliokuwa na uhusiano nao wa kimapenzi walilipwa ili kutozungumzia kashfa hiyo kabla ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2016
Walipoamua kuzungumzia hadharani suala hilo mwaka 2018, utawala wa Trump ulikuwa katika hali ngumu kwasababu ulikabiliwa na hali ambayo ingelimuathiri kisiasa ikiwa ni pamoja na uchunguzi mara mbili wa kihalifu
Hatua ya kwanza ililenga ukiukaji wa sheria za kitaifa na jukumu la Michael Cohen, wakili binafsi wa zamani wa Bwana Trump na "mrekebishaji".
Wakati wa uchunguzi, Cohen alikiri kupanga malipo ya wanawake wawili ili kuwanyamazisha kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Bw.Trump. Malipo hayo yalisemekana kukiuka sheria ya ufadhili wa kampeni na Cohen kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu mwaka 2018
Cohen alidai kuwa Bwana Trump "alimuagiza" kutekeleza malipo hayo lakini hakuna hatua ya kisheria iliyochukuliwa dhidi ya rais. Kwa nini?
Kwanza kabisa, kumshtaki Bwana Trump, waendesha mashtaka walihitajika kuwa na ushahidi wa kuthibitisha kwamba ni kweli alimuagiza Cohen kutekeleza malipo hayo.
Pili, hata kama waendesha mashtaka walikuwa na ushahidi wa kutosha kumfugulia mashtaka Bwana Trump, hatua hiyo inaenda kinyume na sera ya serikali ya Marekani kumfungulia mashtaka rais aliye madarakani, wataalamu wa sheria wanasema.
Kesi ilikamilishwa, sio? La hasha, hilo haijafanyika. Nahapo ndipo mambo yatakuwa magumu.
Ukweli ni kwamba, uchunguzi wa pili wa uhalifu huo wa malipo bado unaendelea New York.
Tunafahamu kuwa Mwanasheria mkuu wa wilaya ya Manhattan Cyrus Vance anachunguza ikiwa shirika la Trump lilifanyia marekebisho rekodi zilizo na uhusiano na malipo hayo.
Kile ambacho hatuna uhakika ni ikiwa Bwana Vance ana ushahidi wowote wa kufungua mashtaka dhidi ya suala hilo.
Nini huenda kikafanyika baadae: Kubadilisha rekodi ya malipo ya kibiashara kwanza njia ya udanganyifu ni hatia chini ya sheria ya New York. Mtu akipatikana na hatia kama hiyo huenda akahukumiwa kifungo cha hadi maka mmoja gerezani.
Lakini, Bwana Vance anakabiliwa na kizingiti cha kisheria
Kuna kikomo cha muda wa miaka miwili kumfungulia mtu mashtaka ya jinai katika Jimbo la New York
"Kwasababu malipo hayo yalifanyika zaidi ya miaka miwili iliyopita, huenda [waendesha mashtaka] hawatafua dafu," Bwana Alonso alisema.
2) Uchuguzi wa udanganyifu wa ushuru na benk
Tunachokifahamu: Ni "hujuma za kisiasa", wakili wa kampuni ya Trump alisema kuhusu uchunguzi wa Bwana Vance mnamo mwezi Agosti mwaka 2019.
Tamko hilo la wackily lilionekana kuwa mbinu ya kujitetea
Wakati huo bwana Vance alikuwa ameomba kupewa nyaraka, zinazofahamika kama subpoena. Alitaka kuona rekodi za kifedha za miaka kadhaa, ikiwamo ile ya Holy Grail - Mapato ya ushuru wa Bwana Trump katika kipindi cha miaka minan
Kuanzia wakati huo, Bwana Trump amejaribu kupinga ombi hilo, akisema mahakamani kwamba hatua hiyo ni sawa na unyanyasaji wa kisiasa. Mwezi Oktoba, Mahakama ya rufaa ilipinga ombi la Bwana Trump,hatua ambayo imemuweka mikononi mwa waendesha mashtaka wanaochunguza mapato yake ya ushuru.
Bwana Vance amesisitiza umuhimu wa rekodi ya mapato ya ushuru ya Trump katika nyaraka zilizoko mbele ya mahakama.
Nini huenda kikafanyika baadae: Bwana Trump anatarajiwa kuwasilisha rufaa ya kupinga ombi la kumtaka awasilishe rekodi yake ya ushuru katika mahakama ya juu zaidi.
Ikiwa Bwana Vance atashidwa kupata rekodi ya Trump ya malipo ya ushuru, kesi ya jinai inaweza kuwa dhahiri au isiwe dhahiri. Kwa vyovyote vile, Bwana anahitaji malipo hayo ya ushuru ili kusonga mbele na uchunguzi wake.
3) Uchunguzi wa udanganyifu wa mali isiyohamishika
Tunacho kifahamu: Mwanasheria Mkuu wa New York Letitia James amekuwa mwiba mchungu kwa Bwana Trump.
Tangu mwezi Machi mwaka 2019, Bwana James amekuwa akiongoza uchunguzi ikiwa shirika la Trump lilifanya udanganyifu wa mali isiyohamishika.
Kwa mara nyingine tena,mzizi wa uchunguzi wake unaelekea kumlenga Cohen ambaye, mnamo mwezi Februari 2019,aliambia bunge kwamba Bwana Trump alikuwa amepandisha thamani ya Mali yake ili kupata mikopo na kupunguza ushuru.
Ushahidi wa Cohen ulimpatia Bi James sababu za kutafuta taarifa kuhusu himaya ya Trump. Sawa na Bwana Vance, Bi James amelazimika kupigania upatikanaji wa taarifa hizo mahakamani
Eric Trump, makamu wa rais mtendaji wa Shirikala Trump na motto wa rais, amemtuhumu kwa kuendesha uchunguzi kwa njia ya ''uonevu''. Licha ya madai hayo, amekubaliana na ombi la kumtaka kudos ushahud akuhusu mienendo ya shirk hilo katika office ya Bi James mwezi Oktoba.
Ni nini hued kikafanyika: Bi James anahitaji ushahidi zaidi pamoja na maelezo ili kuendelea mbele na uchunguzi wake
Akiwa madarakani, Bwana Trump alisema ana kazi nyingi sana na kwamba hana muda wa kushughulikia kesi hizo. Lakini sasa, hawezi tena kutumia sababu hiyo kama kisingizio.
Bi James huenda akamshurutisha Bwana Trump, kufika mbele yake na kujibu maswali chini ya kiapo sawa na alivyofanya mtoto wake