Kigogo Afumaniwa na Mke wa Rafiki Yake Usiku



KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mtumishi mmoja anayefanya kazi idara ya kilimo Kata ya Itumba wilayani Igunga mkoani Tabora, aliyefahamika kwa jina moja la Twalib amenusurika kifo baada ya kutembezewa kipigo alipodaiwa kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa rafiki yake nyuma ya bafu muda saa 2:30 usiku.

Akizungumza na UWAZI, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Lugubu Kata ya Lugubu, Anthony Kapuli alisema tukio hilo lilitokea Novemba 14 na kusababisha tafrani kijijini hapo.


Alisema mtumishi huyo alikwenda nyumbani kwa Paul Martin Kitongoji cha Lugubu magharibi na kumchukua mke wa Paul Martin kisha kumzungusha nyuma ya bafu la Paul na kudaiwa kufanya naye mapenzi.

Alisema wakati wakiwa katika harakati hizo na mke wa rafiki yake ndipo Paul alifika nyumbani kwake alipoingia ndani ya nyumba yake alikuta taa zinawaka pasipo kumuona mke wake.


“Aliamua kwenda chooni kujisaidia ambapo kabla hajafungua mlango wa chooni alisikia sauti nyuma ya bafu lake na alipozunguka aliwakuta mke wake na huyo Twalib wakiwa uchi wa nyama wakifanya mapenzi.


 


“Twalib alimpiga ngumi rafiki yake Paul na kuanguka chini lakini Paul aliinuka kisha kumtembezea kipigo Twalib hadi naye kuanguka chini kisha akamwamuru apige kelele huku akiwa amewadhibiti wote pamoja na mke wake,” alisema.


Alisema baada ya kelele wananchi zaidi ya 200 walifika katika eneo hilo na kukuta watu hao wakiwa uchi ambapo baadhi ya wazee waliomba wavae nguo lakini kundi la vijana liliruhusu mwanamke ndio avae nguo.


Hata hivyo, kundi hilo lilisema kijana huyo achomwe moto ambapo baadhi ya wazee waliomba watuhumiwa wote wawili wapelekwe ofisi ya kijiji hicho.


 


Alisema baada ya kufika ofisini kundi la vijana lilimtaka Twalib alipe Sh. 500,000 za faini na hivyo kulazimika kuweka dhamana ya pikipiki ya serikali anayotumia na kuazimwa fedha na mtu mmoja kwa makubaliano ya kurudisha 650,000.


Alisema mtuhumiwa huyo alidhaminiwa usiku huo na asubuhi yake alirudi ofisini na kulipa Sh. 500,000 kwa mwenye mke kisha kuruhusu kuendelea na majukumu yake ya kazi.


 


Paul Martini alikiri kumkamata ugoni rafiki yake Twalib na kudhibitisha kuwa tayari amelipwa Sh 500,000 na kuwa jumla ya Sh milioni ambayo imetolewa na mtuhumiwa huyo.


Kwa upande wake mtuhumiwa Twalib alipoulizwa juu ya tuhuma hiyo alikiri kukamatwa ugoni na rafiki yake na kudai kuwa shetani ndio alimwingiza kwenye majaribuni.


 


Alisema tayari amelipa Sh milioni moja na kuahidi kutorudia tena tabia hiyo.


Aidha, baadhi ya wananchi Maganga Juma, Mrisho Amoni na Helena Damson walisema kwa nyakati tofauti kuwa mtumishi huyo amekuwa na tabia hiyo kwa muda mrefu jambo ambalo wamedai hawako tayari kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake na kuziomba mamlaka husika kumuondoa katika kata hiyo.

Mtendaji wa Kijiji cha Lugubu, Masaka Chupa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa onyo kwa watumishi na wasio watumishi wenye tabia hiyo kuacha mara moja na badala yake waheshimu ndoa zao na za wenzao ili kuepusha mauaji yasiyokuwa ya lazima.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad