Kimenuka..Polisi yatoa Onyo Wanaotaka Kuandamana...Jeshi la Polisi Halitakuwa na Simile


Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, CP Liberatus Sabas, amesema kuwa jeshi la polisi halitamvumilia mtu yeyote awe kiongozi wa chama au mfuasi, atakayefanya maandamano batili na kama kuna yeyote ambaye hakuridhika na matokeo afuate taratibu za kisheria kudai haki zao kama zipo.


CP Sabas ametoa kauli hiyo hii  Oktoba 31,2020, na kuwasihi akina mama kuongea na watoto wao kwamba, wasithubutu kushiriki katika maandamano hayo na wasije wakarubuniwa na watu ambao hawana nia nzuri na Taifa.


"Nasisitiza kwamba jeshi la polisi halitakuwa na simile kwa yeyote atakayejihusisha na chokochoko hizi ambazo tunaziona zinaanza kuanzishwa na watu hawa ambao hawalitakii mema Taifa hili, nawaomba akina mama mkanye mwanao kwa sababu mwisho wa siku mtoto atakapopata matatizo atakulilia mama, sasa kabla matatizo hayajamfika nakuomba mkanye mwanao", amesema CP Sabas.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Akiingia mtu wa kwanza barabarani,
    anakamatwa na akibaini kuwa amehamassika kwa shinikio la mwana siasa uchwara na kundilao basi hatuulizi tena tunakamata hao wansisa wote na kuwahifadhi panapo stahiki.

    wa kutibiwa tutawatibu ikibidi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad