Kocha wa Yanga Afunguka Baada ya Mechi Dhidi ya Simba

 


Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa wachezaji wake jana Novemba 7 walionyesha bidii kwenye kusaka matokeo kipindi cha kwanza ila mambo yalibadilika kipindi cha pili na kuwa magumu kwetu.


Yanga ilianza kufunga bao la kwanza kupitia kwa Michael Sarpong dakika ya 31 kwa mkwaju wa penalti ikiwa ni bao lake la kwanza ndani ya Yanga kwenye mchezo wake wa dabi na bao lake la tatu jumla.


Kwa upande wa Simba, Joash Onyango ambaye ni beki yeye alisababisha penalti hiyo dakika ya 30 kwa kumchezea faulo Tuisila Kisinda kisha aliweza kusawazisha bao dakika ya 86 kwa kichwa akimalizia kona ya kiungo Luis Miquissone.


Kaze amesema:"Wachezaji walicheza vizuri kipindi cha kwanza ila kipindi cha pili mambo yalikuwa magumu kwa upande wao jambo ambalo liiwafanya waruhusu bao.


"Unajua tulikuwa tunacheza na timu ambayo ina muunganiko kwa muda mrefu jambo ambalo niliwaambia wanapaswa kuwa makini ila kwa walichokifanya ninawapa pongezi."


Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi 10 na kibindoni ina pointi 24 kinara ni Azam FC mwenye pointi 25, Simba nafasi ya tatu na pointi zake ni 20.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad