Lamine Yupo Fiti Kuwavaa Azam FC



BEKI tegemeo na nahodha wa Yanga, Mghana Lamine Moro, hajapata majeraha makubwa baada ya juzi kufanyiwa kipimo cha X-Ray kilichoonyesha hana maumivu yatakayomsababishia kuikosa michezo miwili inayofuatia ya Ligi Kuu Bara.


Beki huyo alitolewa nje katika kipindi cha pili cha mchezo wa Dar es Salaam Dabi iliyopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa timu za Yanga na Simba kutoka sare ya bao 1-1.


 


Katika mchezo huo, Lamine alitolewa kwa kubebwa kwenye machela baada ya kugongana na beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe ambaye yeye aliendelea na mchezo huo.


 


Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafi dh Saleh, alisema kuwa habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa beki wao kipenzi, hajapata majeraha makubwa baada ya jopo la madaktari, linaloongozwa na Shecky Mngazija, kumfanyia vipimo vya X-Ray.


 


Saleh alisema kuwa baada ya kuonekana majeraha hayakuwa ya kiwango kikubwa, beki huyo jana asubuhi alianza mazoezi mepesi ya binafsi huku akiendelea na matibabu katika kujiandaa na michezo ijayo dhidi ya Namungo FC na Azam FC.


 


“Lamine tulimfanyia vipimo juzi Jumatatu na majibu yalionyesha kuwa hakukuwa na hatari yoyote kubwa kwenye goti lake, ulikuwa ni mgongano wa kawaida kati yake na Kapombe.


 


“Ingawa mgongano huo ulimsababishia maumivu makali hapo kabla lakini baada ya vipimo vya X-ray, tumempatia dawa na sasa yuko tayari kuanza mazoezi taratibu.


 


“Hivyo, upo uwezekano mkubwa wa kuwepo sehemu ya kikosi kitakachocheza michezo yetu miwili ya ligi dhidi ya Namungo kabla ya kucheza na Azam,” alisema Saleh.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad