ALIYKUWA Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, amekamatwa na Polisi katika Kaunti ya Kajiado nchini Kenya baada ya yeye na familia yake kuvuka mpaka wa Namanga.
Maafisa wa Uhamiaji walikataa kugonga muhuri nyaraka zilizowasilishwa na mke wa Lema kwa madai hadi wamuone Lema.
Lema aliwaambia maofisa hao kwamba hana hati ya kusaflria kwa sababu alikuwa hasafiri, bali wanaye walikuwa wanakwenda kutafuta shule ya kimataifa. Maafisa waliruhusu mke na watoto kuvuka mpaka, ambapo Lema aliomba kwenda kutafuta fedha za Kenya ili ampe mke wake.
Alipovuka mpaka, Lema na familia yake walingia ndani ya gari la mwanasheria wake, George Luchiri ambapo alisema alitaka ampeleke Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UNHRC) mara tu atakapovuka mpaka. Kwa mujibu wa UNHRC mtu anayetafuta hifadhi hahitaji kuwa na nyaraka za kumwezesha kuingia nchi nyingine.
Kwa mujibu wa tovuti ya The Standard Media ya Kenya, Lema alikuwa na mkewe, Neema Godbless na watoto wao watatu.
Taarifa za Lemakukimbilia Kenya na kuomba hifadhi ya kisiasa, zinakuja takribani siku sita, tangu mwanasiasa mwingine wa upinzani nchini Tanzania kuomba hifadhi ya kisiasa, akihofia usalama wa maisha yake.
Tundu Lissu ambaye alikuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yuko katika makazi ya Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam, akiomba hifadhi kwa kile alichoita, “kuhofia” usalama wake.
Akizungumza na gazeti la hilo, Lema alisema maafisa wa uhamiaji walikataa kugonga muhuri nyaraka zilizowasilishwa na mke wake, kwa madai hadi wamuone yeye.
Amesema, mke wake alipomuita alikwenda, lakini akawaambia hana hati ya kusafıria kwa sababu alikuwa hasafıri na kwamba mke na wanaye walikuwa wanakwenda kutafuta shule ya kimataifa nchini Kenya.
Maafisa hao waliwaruhusu mke na watoto kuvuka mpaka na Lema aliomba kwenda kutafuta fedha za Kenya ili ampe mke wake ambaye alisema angeendelea na safari yeye na watoto.
Maafisa hao wa uhamiaji walitoa taarifa polisi kwamba kuna mtu ameingia nchini humo bila kuwa na nyaraka husika.
“Polisi walitufuatilia na wakatukamata tukiwa Ilbisil na kutupeleka kwenye kituo cha polisi. Sikutaka wamweke pale Lema kutokana na ukaribu wake na mpaka wa Tanzania,” ameeleza mwanasheria huyo akinukuliwa na gazeti la The Standard.
Akieleza sababu za kutotoa hati yake ya kusafıria, Lema amesema, alijua kwa kufanya hivyo, maafisa hao wangemshikilia na kumzuia kuvuka.
“Nimeacha kila kitu nyumbani. Hivyo havina umuhimu kwa sasa. Muhimu ni usalama wangu na usalama wa familia yangu. Nipo na wanangu Allbless, Brilliance na Terrence. Sijui kesho itakuja na nini. Kwa sasa natafuta hifadhi,” Lema ameiambia The Standard.
Mwanasheria huyo amesema atawasilisha taarifa za Lema katika Ubalozi wa Marekani kwani amekuwa akifanya mawasiliano na maafisa wa ubalozi huo.
Aidha, Kenya imesema aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema atarudishwa Novemba 9, 2020 baada ya kwenda nchini humo kutafuta hifadhi kwa UNHRC.
Lema anayeshikiliwa Kituo cha Polisi cha Kajiado amedai maisha yake yapo hatarini. Baadhi ya taarifa zinadai kuwa alikwenda Kenya kuomba hifadhi katika Ubalozi wa Marekani.
Hii imekuja ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema, Tundu Lissu, kuomba hifadhi katika Ubalozi wa Marekani kwa madai kuwa maisha yake yapo hatarini.
Inazua Maswali mengi katika uwajibikaji
ReplyDeletemipakani na Mahaini kupewa Dhamana.
Wamepitaje toka nchini? nani alikuwa
msukaji mipango na mfaikishaji wa suala liza la kusepa..???
Wote walio hamasisha maandamano ni mahaini wa Taifa mpaka itakapo thibitishwa vingine. HAKUNA DHAMANA
SWENDEKA LUPANGO.
DHAMANA INAPELEKEA KUTAFUTA HIFADHI NA UTOROKAJI.. MNAONA YANAJIRI.
ITA WOTE WEKA NDANI. IMARISHENI EXIT CONTROL NA DORIA MIPAKANI NA KIGOMA M.V AMANI MMZAMIAJI ANAE ANDIKA BALUA JUMUIYA YAMADORA AILI YUKO NJE NA ANATUMIA KOMPUTA YAKE PIA ASITOLOOKE KWA BODAODA YUKO HAI PIA WA HAI NA ALIMA NA CHALESI.
ZAIDI YA MIL 60 NI IDADI YA WATANZANIA
Inazua Maswali mengi katika uwajibikaji
ReplyDeletemipakani na Magaidi kupewa Dhamana.
Wamepitaje toka nchini? nani alikuwa
msukaji mipango na mfaikishaji wa suala zima la Magaidi kusepa..???
Wote walio hamasisha maandamano ni mahaini wa Taifa mpaka itakapo thibitishwa vingine.
HAKUNA DHAMANA SWENDEKA LUPANGO.
DHAMANA INAPELEKEA KUTAFUTA HIFADHI NA UTOROKAJI.. MNAONA YANAJIRI.
ITA WOTE WEKA NDANI. IMARISHENI EXIT CONTROL NA DORIA MIPAKANI NA KIGOMA M.V AMANI MMZAMIAJI ANAE ANDIKA BALUA JUMUIYA YAMADORA AILI YUKO NJE NA ANATUMIA KOMPUTA YAKE PIA ASITOLOOKE KWA BODAODA YUKO HAI PIA WA HAI NA ALIMA NA CHALESI.
ZAIDI YA MIL 60 NI IDADI YA WATANZANIA
Swadakta Mdau, Hivyo njia za Panya, Serikali haijajipanga nazo kwa kupandikiza makachero waendeshaboda boda au wabeba mizigo? isitoshe muuza magazeti au maji??
Deleteuongozi wa wilaya na vyombo vya ulinzi na usalama na mawasiliano
MJIPANGEE IPASAVYO.
TANZANIA YETU NI SISI WAKUILINDA
Hongera WaKenya.
ReplyDeleteJe huyu mvunja sheria na taratibu za Uhamiaji anayo Covid-19 certificate ikiambatana na trecing back report?
Atarudishwa mara moja nchini yake.
Mrisho Gambo kiboko.
ReplyDeleteachukua jimbo na kumfanyya mpinzani
kutafuta Economical refuge elsewhere.
Hii Ruzuku, kubwa kuliko.