Tangawizi ni kati ya viungo mahili vinavyochochea ladha nzuri katika vyakula vya aina mbalimbali na hivyo kuwavutia walaji kula chakula husika.
Tangawizi pia inapowekwa kwenye vyakula vigumu kama nyama huifanya ilainike na hivyo kuweza kuiva kwa haraka zaidi.
Leo nataka kukueleza msomaji wangu kuhusu hizi faida nyingine za kutumia juisi ya tangawizi kama ifuatavyo:-
Hutumika kama kituliza maumivu.
Husaidia kuboresha mmeng'enyo wa chakula tumboni.
Huthibiti shinikizo la damu.
Huboresha afya ya kinywa.
Hukinga matatizo ya ngozi hasa chunusi.
Husaidia kukuza nywele (kulinda afya ya nywele.)