Maajabu ya sayari yenye mvua ya mawe na ardhi inayowaka moto



Kama pengine kuna kipindi ushawahi kufikiria kuwa sayari ya dunia tunapoishi sio mahala pazuri, fikiria tena.

Awali dunia haikuwa tofauti na sayari ya K2-14b

Wanasayansi wamebaini sayari nyingine walioipa jina la K2-141b, ambayo mvua yake ni mawe, ikiwa na ziwa la moto la miamba iliyoyeyuka ambalo limechimbwa umbali wa kilomita 100, kasi ya upepo wake ni mara nne zaidi ya kasi ya sauti inavyosafari, upande mmoja ni majivu ya moto yaani lava lakini upande wa pili ni baridi kupita maelezo.

“Hii ni sayari ya kweli ambayo hali yake ya hewa ni kali, ina mawe mengi na upepo wake ni mwingi kweli,” mwanaanga na mwandishi wa vitabu Giang Nguyen ameiambia BBC.

“Sio sehemu ambayo unaweza kuishi kwa raha, lakini ni eneo kimya la kujifunza mambo ya ajabu yanayoonekana duniani tunapoishi!” aliongeza mwanaanga mwenzake Nicolas Cowan.

Wanaanga hao wawili pamoja na wanaanga kutoka India na Canada wamechapisha kitabu chenye uvumbuzi huu wa ajabu.

‘Karibu katika Sayari ya moto’Sayari hii na nyota zake zina miaka 202 kutoka katika mwanga

Sayari ya K2-141b, inapatikana umbali wa miaka 202 ya nuru kutoka sayari ya dunia. Katika sayari hii ya ajabu, mwaka mmoja unakamilika chini ya saa saba kulingana na wanasayansi.

Na kwasababu ya jinsi ilivyo, mchana ni joto kali na usiku kuna baridi kali.

“Ni sayari iliyotengenezwa kwa moto,” wamesema wanasayansi wanaochunguza na kutayarisha taarifa wakati wa utafiti kutoka Taasisi ya Sayansi India huko Kolkata, Chuo kikuu cha York Toronto, Canada, na chuo kikuu cha McGill kilichopo Montreal, Canada.

Ni sayari ya “nguvu na ya kufurahisha”, kwasababu, ingawa sio kubwa kushinda sayari ya dunia tunayoishi, nguvu ya uvutano ni mara tano kuliko dunia.

Ingawa sayari ya K2-141b iligunduliwa kwa mara kwanza 2018 na wanaanga wa Kepler Space Telescope, sasa hivi ndio wanaanga wanagundua maajabu ya sayari hiyo ya kipekee.

Hali ya hewa iko nanma gani?Fikiria moto ardhini huku mawe yenye barafu yakianguka sakafuni ndiposa utaelewa

Ingawa mzunguko wa sayari ya K2-141b ni ndani ya saa kadhaa, haisogei moja kwa moja kama ilivyo kwa dunia.

“Hii ina maanisha kuwa theluthi mbili ya sayari hiyo inamwilikwa na jua na kiwango chake cha joto kinaweza kufika hata nyuzi joto 3,000 za selsiasi,” amesema Profesa Cowan.

Pia kitu kingine tofauti, sehemu nyingine iliyosalia ya sayari hiyo huwa kila wakati ipo kwenye giza na nyuzi joto upande huo inaweza kushuka hadi -200 za selsiasi.

‘Sayari ya kushangaza lakini maajabu yake ni ya kweli’Ni kama mvua lakini mawe yake husukumwa na upepo mkali
Ni kama mvua lakini mawe yake husukumwa na upepo mkali
“Kile unachostahili kutilia maanani ni kwamba kila kitu katika sayari hii kimetengenezwa kwa mawe,” amesema Profesa Cowan.

Hii ni kwasababu joto la upande wa nje wa sayari wakati wa mchana “liko juu sana kiasi kwamba linayeyuka na kuwa mawe. Inashangaza kweli lakini ndio ukweli wa mambo ulivyo.!”

“Lakini ile sehemu ya giza nyakati za usiku haina joto, na hiyo ndio sababu usiku kunakuwa na baridi ya ajabu mno,” aliongeza.

Pengine kuna chochote kilichokoseka?Hakuna mafunzo mengi kutoka kwa sayari zilizopo mbali nasi
Hakuna mafunzo mengi kutoka kwa sayari zilizopo mbali nasi
Bila shaka unajiuliza uvumbuzi huu una umuhimu gani kwa binadamu?

“Utafiti wa sayari ya K2-141b unatusaidia kuelewa historia ya zamani ya hali ya hewa ya dunia, jinsi wakati fulani ilivyokuwa joto sana,” amesea Mwanaanga Nguyen.

“Sayari za moto zinatupa fursa ya kutathmini hali ya sasa ya sayari yetu,” aliongeza Profesa Cowan.

“Sayari zenye miamba ikiwemo tunayoishi ya dunia zilianza kwa hali ya hewa ya joto la juu sana lakini baadaye hali hiyo ikaanza kupoa.”

Hivyo basi, kufahamu mengi kuhusu sayari ya K2-141b, kunaweza kuimarisha zaidi uelewa wetu wa vile hali inavyoweza kuwa duniani.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad