Nchini Ufaransa kwa mara ya kwanza kumeripotiwa maambukizi mapya ya virusi vya corona yanayopindukia 52,500 ndani ya saa 24.
Idadi hiyo imeongezeka kwa maambukizi 500, ikilinganishwa na kiwango cha juu cha hapo awali, kama ilivyoripotiwa na mamlaka ya afya nchini humo.
Takriban asilimia 20.6 ya watu waliopimwa virusi hivyo wamethibitishwa kuambukizwa.
Aidha mamlaka za afya zimeripoti vifo 400 zaidi vinavyotokana na virusi vya corona, ndani ya siku moja katika hospitali tofauti.
Kiwango hicho cha maambukizi nchini Ufaransa ni kikubwa kushuhudiwa tangu kuzuka kwa maambukizi hayo mnamo mwezi Machi.
Hali inaelezwa kuwa imezidi kuwa mbaya katika wiki za hivi karibuni.
Tangu Ijumaa iliyopita, serikali ya Ufaransa ilianza kutelekeleza kote nchini hatua kali za kupambana na virusi hivyo, na zinatarajiwa kuweko hadi mwanzoni mwa mwezi Desemba.