Mahakama Yaamuru Mali za Nabii Bushiri Kushikiliwa

 


Nabii Milionea wa Malawi, Shepherd Bushiri anayehubiri nchini Afrika Kusini na mkewe Mary wamejikuta kwenye wakati mgumu baada ya mahakama ya Afrika Kusini kuamuru kushikiliwa kwa nyumba yao baada ya kukwepa kesi ya dhamana.


Kasri hiyo ya kifahari iliyopo karibu na Mji wa Pretoria ina thamani ya randi milioni 5.5 za Afrika Kusini sawa na dola 350,000 au pauni 260,000, kwa Tsh ni 810,353,950 kwa mujibu wa taarifa.




Jaji aliwaamuru Nabii Bushiri na mke wake kutoa stakabadhi za nyumba wakati mahakama hiyo ilipowapa dhamana kufuatia tuhuma za utakatishaji wa fedha na ufisadi zinazowakabili.


Hatua hiyo ya mahakama inakuja wakati Mchungaji huyo maarufu akikabiliwa na mashtaka 419 na utakatishaji fedha nchini Afrika Kusini.


Wakati huo huo Mahakama ya Malawi ilimuachilia huru Nabii Shepherd Bushiri na mke wake baada ya kukamatwa mapema leo.


Afrika Kusini bado inawataka Bushiri na mke wake ambao walitorokea nchini kwao Malawi warejee Pretoria kukabiliana na mashtaka dhidi yao.




Nabii Shepherd Bushiri na mke wake, Mary Bushiri ambaye pia ni Nabii walikanusha tuhuma dhidi yao mwishoni mwa juma, kupitia ujumbe walioutuma kwenye mitandao ya kijamii wakidai walikuwa nchini Malawi kwa kuhofia usalama wao.


Tayari Afrika Kusini imekwishatoa kibali cha kuwakamata wawili hao na wanataka mamlaka za Malawi ziwarejeshe nchini Afrika Kusini kukabiliana na kesi yao .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad