Wanadiplomasia wamesema makombora yamerushwa katika mji mkuu wa Eritrea, Asmara, wakati mapigano katika jimbo la kaskazini la Tigray yakionekana kuvuka mpaka hadi katika nchi jirani.Waangalizi wanasema mapigano hayo yamezua hofu na wasiwasi mkubwa.
Takriban makombora matatu yalilenga uwanja wa ndege mjini Asmara, saa chache tu baada ya uongozi katika jimbo la Tigray kuonya kuwa unaweza kufanya mashambulizi.
Uongozi wa Tigray unaishtumu Eritrea kwa kuishambulia kutokana na mwaliko wa serikali ya Ethiopia, tangu vita katika jimbo hilo la kaskazini kuanza mnamo Novemba 4.Hata hivyo hakujatangazwa taarifa zozote za kutokea uharibifu au vifo.