Mamba walivyoua watu 19 ndani ya miaka minne



Watu 19 wamepoteza maisha kwa kuliwa na mamba wakati wakifanya shughuli mbalimbali ndani ya Ziwa Victoria kwa kipindi cha miaka minne huku watu wanane wakijeruhiwa.

Ongezeko hilo limekuja baada wa watu wawili ndani ya miezi miwili kupoteza maisha kwa kuliwa na mamba wakioga ndani ya Ziwa Victoria

Oktoba 24 mwaka huu, Reulensia Igayo (28) mkazi wa Kijiji cha Kisaba Wilaya ya Buchosa alipoteza maisha kwa kuliwa na mamba.

Pia, dereva wa boti ya abiria ya Mv Mwanzo inayofanya safari zake kati ya Kijiji cha Kanyala na visiwa vya Kasalazi, Gembale, Nyamango na Soswa, Revocatus Mtani(35) alipoteza maisha jana baada ya kuliwa na mamba wakati akioga ziwani katika Kijiji cha Kanyala Halmasahauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

Mkuu wa wilaya hiyo, Emmanuel Kipole alisema jitihada za kupata mabaki ya mwili wa Mtani zinaendelea.

“Ni kweli tukio limetokea la mtu kupoteza maisha kwa kuliwa na mamba, Serikali itashirikina na idara ya wanyapori ili kwenda kuwavuna mamba hao,” alisema Kipole.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad