Mambo 9 ya kushangaza kuhusu Mwezi na sababu za Marekani



Umbo la mwezi hubadilika na hata rangi yake, lakini tangu jadi binadamu amekuwa akivutiwa na maumbile yake. Kuna Mwezi Mpevu, Mwezi Mwandamo, Hilali na hata wakati mwezi hupatwa na jua.

Mwezi mwekundu unapanda nyuma ya Saentis (2502m) Alpstein, nchini Uswizi

Hapa tumekuandalia mambo tisa ya kushangaza kuuhusu Mwezi.

1. Mwezi si tufe
Mwezi una umbo la yai. Ukiuangalia kile unachokiona ni moja ya sehemu ndogo za kando. Si kitu kilicho na umbo lililo sawa kwa uzito- eneo lake la kati la uzito haliko kabisa katikati mwa Mwezi bali karibu kilomita 2 kutoka sehemu ambayo inadhaniwa kuwa ndicho kitovu cha Mwezi.

2. Hatuuoni mwezi wote.
Kwa kila wakati fulani sisi huona asilimia 59 ya Mwezi. Uliobakia asilimia 41 hauwezi kuonekana kutoka duniani. Na kama huwezi kuamini, kama unaweza kwenda anga za mbali na kusimama eneo hilo la asilimia 41 huwezi kamwe kuiona dunia!

3. Mwezi wa Samawati ulitokana na volkanoMlipuko mwa mlima kwa jina Anak Krakatau (Mwana wa Krakatoa) Julai 2018 nchini Indonesia
Mlipuko mwa mlima kwa jina Anak Krakatau (Mwana wa Krakatoa) Julai 2018 nchini Indonesia
Umewahi kusikia kuhusu Mwezi wa Samawati au Buluu ambao kwa Kiingereza huitwa Blue moon? Matumizi ya msemo huu yanaaminika kuanzia mwaka 1883 kufuatia kulipuka kwa mlima wa volkano wa Krakatoa nchini Indonesia. Vumbi kubwa lilijaa angani hivi kwamba wakati uliuangalia Mwezi, ulionekana kama ulikuwa na rangi ya samawati.

Kwa kweli ni kitu ambacho hakikuwa cha kawaida ndio kikachangia msemo “once in a blue moon” ikimaanisha kitu ambacho ni nadra sana kutokea.

 

4. Mpango wa Marekani kuulipua Mwezi

Marekani wakati mmoja ilitaka kuulipua Mwezi kwa kutumia bomu la nyuklia. Marekani ilikua inataka sana kulipua bomu la nyuklia mwezini.

 

Lengo lilikuwa ni kuonyesha ubabe wa Marekani kuiwezesha kuitia kiwewe Urusi na washirika wake wakati wa vita baridi, hasa baada ya Muungano wa Usovieti kuongoza katika jitihada za kupeleleza na kutalii anga za juu, hasa baada ya kurusha satelaiti ya kwanza kwenye mzingo wa dunia, satelaiti ya Sputnik 1 mnamo 4 Oktoba 1957.

 

Wataalamu walikuwa pia wanachunguza madhara ambayo yangesababishwa na mlipuko mkubwa wa nyuklia kwenye mazingira.

 

Mradi huo wa siri ulipewa jina ‘A Study of Lunar Research Flights‘, au ‘Project A119‘ na ulianzishwa mwaka 1958. Utafiti hata hivyo ulikuwa umeanza kisiri mwaka 1949 katika kituo cha utafiti kuhusu silaha cha ARF katika Taasisi ya Teknolojia ya Illinois.

 

Mlipuko wa bomu hilo ungekuwa mkubwa sana hivi kwamba ungeonekana kutoka duniani.

Mpango huo haukutekelezwa kutokana na wasiwasi kwamba raia hawangeupokea vyema na pia hatari kwa binadamu iwapo mpango huo ungeenda mrama na ulifutwa rasmi Januari 1959.

 

Aidha, kiongozi wa mradi huo Leonard Reiffel alihofia hatua kama hiyo ingekuwa hatari kwa juhudi za baadaye za kupeleleza zaidi kwenye Mwezi na pia mpango wa kuwapeleka binadamu wakaishi huko.

Taarifa za kuwepo kwa mpango huo zilifichuliwa mwaka 2000.

5. Kupatwa kwa mwezi ‘kulikosababishwa na joka’Kupatwa kwa jua zamani China kuliaminika kutokana na mwezi kumezwa na jua
Maelezo ya picha,Kupatwa kwa jua zamani China kuliaminika kutokana na mwezi kumezwa na jua
Imani za kale za Kichina zilisema kuwa kupatwa kwa jua kulisababishwa na joka kulimeza jua.

Kuzuia hilo watu walipiga kelele sana wakati wa kupatwa kwa jua kumfanya joka aogope na atoroke.

Pia waliamini kuwa chura mkubwa aliishi kwenye Mwezi akiketi juu ya shimo kubwa. Mashimo makubwa kwenye Mwezi hayakusababishwa na wanyama wowote bali yalisababishwa na mawe makubwa ya anga za juu kuugonga mwezi takriban miaka bilioni 4.1 iliyopita.

6. Mwezi unapunguza kasi ya dunia.
Wakati mwezi unakaribiana sana na dunia kile kinachaoitwa Perigee hutokea. Hii inamaanisha kuwa nguvu za kuzunguka kwa dunia hutwaliwa na Mwezi kidogo kidogo hali ambayo husababisha dunia kupunguza kasi yake kwa karibu milisekunde 1.5 kwa kila karne moja.

 

7. Mwangaza wa mwezi
Jua lina mwangaza wenye nguvu mara 14 zaidi ya ule wa Mwezi unapokuwa mpevu. Ili Mwezi mpevu upate kuwa na mwangaza sawa na wa jua unahitaji kuwa na Miezi 398.110. Wakati wa kupatwa kwa Mwezi wakati mwezi unaingia kwenye kivuli cha dunia viwango vya joto mwezini vinaweza kushuka hadi karibu nyuzi joto 500F (260 celsius) katika kipindi cha chini ya dakika 90

8. Leonardo da Vinci aligundua kuwa mwezi haukuwa na umbo la hilaliHilal Bayonne, New Jersey Julai 2018

Wakati Mwezi unaonekana kuwa umbo la hilali, kile tunachokiona ni mwanga wa jua ukimulika sehemu ya Mwezi. Eneo jingine la mwezi halionekani vizuri, kulinngana na hali ya hewa. Leonardo da Vinci ndiye mtu wa kwanza anayejulikana kugundua kuwa mwezi haukuwa unapungua au kuongezeka. Ni kuwa sehemu yake nyingine ilikuwa imefichwa.

9. Kutoa majina kwenye MweziShimo kubwa la Giordano Bruno kwenye Mwezi lililo na upana wa kilomita 22
Maelezo ya picha,Shimo kubwa la Giordano Bruno kwenye Mwezi lililo na upana wa kilomita 22
Muungano wa Kimataifa wa Anga za Juu ndio huyapa majina mashimo yaliyo kwenye Mwezi na pia mawe, sayari na vitu vingine vinavyopatikana anga za juu. Mashimo makubwa kwenye mwezi yamepewa majina ya wanasayansi, wasanii na wapelelezi maarufu. Mashimbo yanayopatikana karibu na shimo kubwa la Apollo hupewa majina ya Wamarekani na yale yanayozunguka shimo kubwa la Mare Moscoviense hupewa majina ya Warusi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad