Ugonjwa wa kisukari ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza, ambayo husababishwa baada ya kongosho kushindwa kutengeneza 'insulin' ya kutosha ndani ya mwili.
Insulin ni homoni ambayo kazi yake kubwa ndani ya mwili ni kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.
Sasa leo naomba nikwambie wewe msomaji wangu haya mambo saba ambayo ukiyafanya kila siku unaweza kujiweka mbali na ugonjwa huu wa kisukari.
1. Kuwa na uzito wa kawaida
Zingatia kuwa na uzito unaoendana na wewe kiafya kwani hali ya uzito mkubwa huweza kuwa chanzo cha tatizo hili la kisukari. Unapokuwa na uzito wa kawaida unaambiwa kuwa utakuwa umejiweka mbali na ugonjwa wa kisukari kwa asilimia 6.
2. Zingatia ulaji bora
Unapaswa kula chakula kwa kufuata taratibu bora za kiafya ikiwa ni pamoja na kuzingatia ulaji wa matunda pamoja na mbogamboga.
3. Kunywa maji ya kutosha
Unashauriwa kunywa maji ya kutosha kadri uwezavyo, unatakiwa kunywa angalau glass 7 hadi 8 kwa kila siku
4. Usisahau kufanya mazoezi
Mazoezi ni muhimu kwa kila mtu, hivyo kama wewe unapenda kuepukana na ugonjwa huu wa kisukari ni vyema kujitahidi kunywa maji ya kutosha kila siku.
5. Epuka msongo wa mawazo
Mawazo nayo yanapozidi huweza kuwa chanzo cha tatizo hili la kisukari, hivyo jitahidi kuepuka tabia ya kuwa na msongo wa mawazo mara kwa mara ili kujiweka mbali zaidi na ugonjwa wa kisukari.
6. Pata muda wa kutosha wa kulala
Kulala nako ni muhimu kwa afya zetu wanadamu pia ni moja ya njia ya kufanya kuepuka na ugonjwa huu wa kisukari
7. Fanya uchunguzi wa afya mara kwa mara
Jitahidi kujenga utaratibu wa kuchunguza afya yako mara kwa mara ili iwe rahisi kugundua matatizo yako ya kiafya mapema kabla ya tatizo kuwa kubwa zaidi.