Mamia Waandamana Ufaransa kupinga Sheria mpya ya usalama


Maelfu ya watu wameandamana katika miji ya Ufaransa kupinga rasimu ya sheria ambayo itaweka mipaka juu ya kuwarekodi maafisa wa polisi wanapokuwa kazini, hatua ambayo imetajwa kama ya kubinya uhuru wa vyombo vya habari. 

Mnamo siku ya Ijumaa, bunge liliidhinisha sheria ya usalama iliyofanyiwa marekebisho ambayo inasema ni kosa kuchapisha picha za maafisa wa polisi walioko kazini kwa nia ya kuwadhuru kimwili au kisaikolojia.Mkusanyiko mkubwa wa watu wasiopungua 7,000 ulikuwa karibu na mnara wa Eiffel mjini Paris huku polisi ikikabiliana na baadhi ya watu kufuatia rabsha zilizotokea baada ya maandamano hayo.


Miongoni mwa watu walioshiriki maandamano hayo ni pamoja na vugu vugu la Vizibao vya njano na baadhi ya watu waliobeba bendera za vyama vya kikomunisti na chama cha kijani, pamoja na chama cha wafanyikaz

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad