Marekani kuondoa wanajeshi zaidi Afghanistan, Iraq



Maafisa katika serikali ya Marekani wamesema kwamba rais Donald Trump anatarajiwa kupunguza idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan kwa zaidi ya nusu, na kubakisha wanajeshi 2,500 nchini humo, ifikapo Januari 15. 


Kulingana na shirika la habari la Associated press, amri hiyo ya rais Trump hata hivyo haitatimiza ahadi yake ya kuondoa kabisa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. 


Hatua hiyo ilipingwa na washauri wa kijeshi na kidiplomasia. Pentagon inatarajiwa pia kupunguza wanajeshi wa Marekani nchini Iraq kufikia 2,500, ikiwa ni punguzo la zaidi ya wanajeshi 500. Hatua hiyo inachukuliwa baada yar ais Trump kuwafuta kazi maafisa wa ngazi ya juu wizara ya ulinzi na kuteua wale wanaounga mkono maamuzi yake. 


Maafisa wa serikali wamesema kwamba viongozi wa jeshi waliarifiwa wikendi iliyopita kuhusu mpango huo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad