Kikitoka kizazi cha msanii Alikiba na Simba wewe ndiyo mfalme, hiyo ni kauli ambayo ameitoa msanii wa BongoFleva Marioo kumwambia msanii mwenzake Aslay Isihaka ikiwa ni ishara ya kumpa heshima na kukubali anachokifanya.
Ni mara chache sana kuona wasanii wakitoa heshima kwa wasanii wenzao wakiwa bado wapo hai, mara nyingi huwa wanafanya hivyo endapo akiwa hayupo duniani, ila hii imekuwa tofauti na msanii Marioo ambaye ametoa ya moyoni kuhusu Aslay.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Marioo amepost picha tano za msanii Aslay huyo kisha ameandika kuwa "Inaweza ikawa jamii inakupa heshima na ukubwa ila mimi nadhani unastahili zaidi, kikitoka kizazi cha kina Kiba na Simba wewe ndiyo mfalme, heshima".
Aslay ni mmoja wa wasanii wa BongoFleva ambao wana historia ya kuanza muziki wakiwa na umri mdogo zaidi, wasanii wengine ni Mr Blue, Young Dee, Dogo Janja na Young Killer.