Katika shitaka la kwanza la kutosajili JamiiForums kwa kikoa cha DO-TZ, Maxence amekutwa hana hatia
Katika shtaka la pili, Mahakama imemkuta na hatia na kumuachia kwa masharti ya kutofanya kosa kama hilo kwa muda wa mwaka mmoja
Shitaka la pili lilihusisha Jeshi la Polisi kumtaka Maxence Melo kutoa taarifa za wanachama wa JamiiForums waliofichua uhalifu uliofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa CRDB
Mshitakiwa namba mbili, Mike Mushi amekutwa hana hatia makosa yote Mawili. Hakimu Huruma amesema, Mshitakiwa huyo alikuwa kama Msindikizaji kwenye hii kesi