Mazungumzo ya Libya yamalizika bila kupendekeza serikali ya mpito



Pande hasimchini Libya zimekamilisha mazunguzmo ya wiki moja yaliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa bila ya kufikia makubaliano ya kuunda serikali ya mpito ambayo ingeongoza nchi hiyo kuelekea uchaguzi mkuu wa Disemba mwaka unaokuja. 




Kaimu mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya Stephanie Williams amewaambia waandishi habari mjini Tunis, kuwa mkutano huo uliowakutanisha wajumbe 75 wa Libya haukujadili majina ya watu watakaounda serikali lakini mazungumzo yaliyofanyika yanatia moyo. 




Mazungumzo hayo yalifanyika chini ya shinikizo kali kutoka jumuiya ya kimataifa baada ya Umoja wa Mataifa kufanikiwa kupatikana mkataba wa kusitisha mapigano kati ya pande hasimu nchini Libya mwezi uliopita.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad