MWENYEKITI wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amewataka viongozi wa kidini kutumia ndimi zao vizuri, kukubaliana na maslahi ya Tanzania kwanza na wasikubali kukichoma moto kichaka kinachowahifadhi.
Amesema hisia za wanasiasa kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu haziwezi kuelezwa kwa maneno, bali watu wote wenye upendo na Tanzania wanaweza kuziona hisia hizo.
Ameongeza: “Maneno hayatoshelezi kuelezea hisia, labda kwa kupitia nafsi. Hisia zetu kwa ujumla kuhusu mchakato wa tukio lililoitwa Uchaguzi Mkuu wa 2020, haziwezi kuwakilishwa kwa maneno, lakini wote wenye nia nzuri na mama yetu #Tanzania wanaweza kusikia au kuelewa hisia za wengi kwa muda huu.
Amesisitiza kwamba miaka 28 chama chake kimekuwa kikiimba wimbo wa kupata Tume Huru ya Uchaguzi na kwamba sasa gharama zake zimekuwa kubwa.