Mbowe, Zitto na Lema waachiwa kwa dhamana

 


Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ni kati ya viongozi wa upinzani walioachiwa kwa dhamana leo Jumanne Novemba 3, 2020.


Wengine walioachiwa ni wajumbe wa kamati kuu ya Chadema,   Godbless Lema na Boniface Jacob ambao pamoja na Mbowe walikamatwa na polisi usiku wa kuamkia Novemba 2, 2020 wakiwa kwenye kikao. Zitto alikamatwa leo mchana alipokwenda kuwatembelea kina Mbowe polisi.


Leo jioni Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa aliieleza Mwananchi Digital kuwa viongozi hao wataachiwa kwa dhamana kwa kuwa alikuwa ametoa maelekezo hayo, na baadaye wakili wa Chadema John Mallya alisema viongozi hao wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti polisi Novemba 5, 2020 saa 3 asubuhi.


Mallya amesema viongozi hao wameachiwa baada ya kujidhamini wenyewe na kutakiwa kutotoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam na kuhakikisha wanaripoti kituoni hapo tarehe waliyopangiwa.


Oktoba 31, 2020,  Mbowe na Zitto wakiwa pamoja na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Tundu Lissu walitangaza maandamano ya amani yasiyo na ukomo nchi nzima kuanzia Novemba 2, 2020 kupinga mchakato wa uchaguzi mkuu wakitaka urudiwe.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad