Mbunge Babu Tale aanza kazi jimboni kwake


Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamisi Shabani Babu Tale tayari ameingia kazini na jana amefanya ziara katika Tarafa na Kata za Ngerengere, Mkurazi, Matuli na Gwata Wilaya ya Morogoro Vijijini.
Aliambatana na Wataalamu wa Maji Ardhini kutoka Wizara ya Maji ili kuchuguza na kuanza taratibu za uchimbaji wa visima vyenye maji safi na salama ili kuondoa kero kubwa ya muda mrefu ya tatizo la maji kwa Wakazi wa kata hizo lilodumu kwa muda mrefu.

"Kwanza nawashukuru sana wataalamu wa maji Ardhini pamoja na @jumaa_aweso kwa kunikutanisha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Anthony Sanga, na kwakipekee namshukuru sana Mwenyekiti wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchagua watu ambao wanafikika na wanatatua kero za watu”

"Wataalamu hawa wameahidi kutuchimbia visima 7 impala 8 katika kata moja, leo hii nimepeleka maji Ngerengere kwasababu kilio kikubwa cha wanangerengere ni maji"- Tale


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad