Mbunge wa CHADEMA atoa ushauri kwa viongozi wake "Siwezi Kususia Matokeo"

 


Mbunge mteule wa jimbo la Nkasi Kaskazini, kupitia CHADEMA, Aida Khenani, amewataka viongozi wa chama chake kufuata sheria kama kuna maeneo wameona kuna dosari, lakini kwa upande wake hawezi kususia matokeo wala kukataa kuapishwa kwa ajili ya heshima ya wananchi wake waliomchagua.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 9, 2020, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, na kusisitiza kuwa msimamo wa awali wa chama chake kabla ya uchaguzi haujaanza, viongozi walisisitiza suala la kutokususia uchaguzi na hivyo yeye anashikilia msimamo huo.


"Chama changu kilinipa msimamo kwamba hatutasusia uchaguzi na mimi nilishiriki na leo imekuwa ni vigumu sana kurudi kwa wananchi kuwaambia nasusia matokeo, kama sikususia uchaguzi siwezi kususia matokeo, lakini maeneo ambayo wanafikiri kuna dosari nashauri waendelee kufuata utaratibu wa kisheria na haki itatendeka", amesema Aida.


Aidha Aida amesema kuwa, "Mimi nikiambie chama changu, sijahama CHADEMA na wala sitegemei kuhama mimi ni mbunge mteule ambaye nilipitia CHADEMA kwa hiyo nitawatumikia wananchi kwa imani ambayo waliniamini, labda chama changu kitakavyoamua kama itakuwa vinginevyo basi itafahamika".

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad