Mchakato wa kukabidhi madaraka watumbukia katika vurumai Marekani

 


Utawala wa Donald Trump umesababisha hali ya sintofahamu, kwa kuwazuia maafisa wa serikali kushirikiana na watu wa rais mteule Joe Biden, huku mwanasheria mkuu William Barr akiiruhusu wizara ya sheria kufanya uchunguzi juu ya maadai ya wizi wa kura bila ya ushahidi wowote. 

Baadhi ya wajumbe wa chama cha Republican, ikiwa pamoja na kiongozi wa baraza la seneti Mitch McConell wanaunga mkono hatua za rais Trump za kuendelea kuyapinga matokeo ya uchaguzi  ambapo mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden alishinda. 


Baraza maalumu la wapiga kura linatarajiwa kuuidhinisha rasmi ushindi wa Biden mwezi ujao na anatazamiwa kuapishwa mnamo mwezi  Januari. 


Wakati huo huo rais Trump hapo jana Jumatatu alimwachisha kazi waziri wake wa ulinzi Mark Esper.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad